Wakurugenzi wa halmashauri nchini wametakiwa kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kuwapanga wamachinga kutekelezwa bila kutumia mabavu.


Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ummy Mwalimu wakati wa kufungua kikao kazi cha siku mbili na wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Alisema ni vyema wakatumia mwezi mmoja uliotolewa kuwaelimisha na kuwashirikisha wamachinga katika kupanga miji.


Septemba 13 mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan alitoa maelekezo Kwa halmashauri za Majiji na manispaa kuwapanga wamachinga na Waziri Mkuu alitoa maelekezo ya kutekeleza hilo ndani ya mwezi mmoja.


Alisema Wakurugenzi wanapaswa kuwa makini na njia wanazozitumia kuwatoa wamachinga kuwa ziwe ni zile zinazingatia utu, heshima na thamani ya wafanyabiashara wadogo wadogo.


“ Nataka kusisitiza tutumie mwezi mmoja huu kutoa elimu Kwa wamachinga na kuhakikisha wanashirikishwa katika kupanga miji.”


“ Tujitahidi sana kutotumia nguvu na mabavu, tutekeleze maagizo ya Rais huku tukizingatia sheria, taratibu na kanuni na kuwashirikisha na kuandaa maeneo ya kuwapeleka.”


Ummy pia aliwataka kutengwa maeneo ya wafanya biashara ambayo wananchi wanafika kiurahisi

Share To:

Post A Comment: