Wachimbaji wa madini nchini wameaswa  kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa upendo ili kuepuka migogoro ya mara kwa mara na kesi zisizoisha katika maeneo ya uchimbaji.


Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Madini Mhe.Prof.Shukrani Manya wakati akitatua  mgogoro wa wa umiliki  wa mgodi wa uchimbaji dhahabu katika machimbo ya matongo Wilayani Ikungi.

“Maelekezo ya Serikali ni kwamba mnapaswa kuchimba kwa usalama lakini pia kwa kupendana,Wizara yetu sio ya migogoro bali tupo hapa kwa ajili ya kutoa huduma kwa wachimbaji ili kuleta tija katika masilahi yenu binafsi na maendeleo ya uchumi wa taifa hili”,amesema.

Akitoa elimu kwa wachimbaji hao kuhusu umuhimu wa leseni Prof Manya alisisitiza wachimbaji hao kufika kwa afisa madini mkazi ili waombe leseni za uchimbaji wa madini.

“Kabla ya kuanza kuchimba madini unaitaji kukatia leseni eneo hilo hili ujulikane unamiliki ardhi juu na madini yaliyoko chini ili yaweza kuwa ni halali yako”amesisistiza

Aidha Naibu Waziri Prof.Manya aliwaasa wachimbaji na wamiliki wa leseni  kumshirikisha Afisa madini mkazi katika kila jambo wanaloona hawalielewi na lina utata  ili  kupunguza migogoro.

Katika hatua nyingine amewata wachimbaji hao kushiriki katika masuala ya kijamii ili kijiji icho kinufaike na uwekezaji  wao.

“Nawaasa changieni madawati katika elimu,tumekuja kutafuta riziki katika kijiji hiki mkiondoka hapa Mashimo yatabaki hapa kwa iyo wenye Mwalo,mwenye karai na mwenye leseni ikitokea hoja ya kijiji iwe hoja yenu wote”ameeleza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Bw.Jerry Muro altoa wito kwa wachimbaji hao kudumisha Amani na kujikinga na uviko-19 na pia kuwaamasisha kujitokea kupata chanjo kwani wamesogeza vituo katika eneo hilo
Share To:

Post A Comment: