Na Elizabeth Joseph, Iringa.


PONGEZI yatolewa kwa Serikali,Watafiti,pamoja na Vikosi kazi katika jitihada za kulinda maji ya Mto Ruaha kukauka.


Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Ikolojia katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo mkoani Iringa Dkt, Halima Kiwango wakati akiongea na Waandishi wa habari Wanawake kutoka mikoa mbalimbali nchini walipotembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha.


Alisema kuwa kutokana na changamoto ya kukauka maji ya mto huo iliyoanza kuonekana mwaka 1993 Serikali pamoja na wadau wengine wamekuwa wakifanga jitihada ya nini kifanyike katika kutatua changamoto hiyo ambapo toka Novemba mwaka 2019 kumekuwa na mabadiliko katika mtiririko wa maji bila kukauka hata kipindi cha kiangazi licha ya wingi wake kupungua.


"Toka 1993 mto huu kwa mara ya kwanza na umekuwa ukiendelea kukauka kila mwaka kwa takribani miezi miwili hadi mitatu,hali hiyo imekuwa ikileta athari katika Afya ya Ikolojia ya Ruaha mfano kipindi Cha kiangazi Wanyama wanakosa maji na afya zao kudhoofika hivyo kusababisha kushambuliwa na Magonjwa...................


"Mwaka 2017 tulipata tukio ambalo tunasema ni la kihistoria, mto ulikauka kwa muda mrefu Wanyama walikufa hasa Viboko ambao walikufa 66  na ulitokea ugonjwa wa Kimeta ambao hutokea panapokuwa na ukame mkali"alieleza Dkt,Kiwango.


Aidha aliiomba Jamii hasa inayozunguka Mto huo kuulinda na kuutunza vizuri ili kulinda uhai wa Wanyama kwakuwa ndio tegemeo lao katika kunywa maji pamoja na binadamu wengine kutumia katika shughuli mbalimbali za kilimo ikiwemo matunda na mbogamboga.


"Tukilinda vyanzo vya maji tutapata faida sisi binadamu na Wanyama pia lakini tukiharibu hasara ni kwa wote hivyo tuweke jitihada katika kutunza na kulinda mto wetu ili usije kukauka tena"Aliongeza Dkt,Kiwango.


Share To:

Post A Comment: