Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Zainab Terack akifungua mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wasindikaji wa korosho na bidhaa za korosho katika mkoa huo.Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Waanishi wa habari wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Zainab Terack wakati akifungua mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wasindikaji wa korosho na bidhaa za korosho katika mkoa huo.

******************************

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe.Zainab Terack ameipongeza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa maandalizi mazuri ya mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni wasindikaji wa korosho na bidhaa za korosho katika mkoa huo.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo RC Terack amewataka TBS kuyafanya mafunzo hayo kuwa endelevu na kuongeza nguvu katika kuboresha mahusiano na halmashauri za Mkoa wa Lindi hasa kushirikiana kwa karibu na ofisi za wakurugenzi wa halmashauri.

Aidha RC Tereck amewataka wajasiriamali ambao wanapokea mafunzo hayo waweze kuwa wasikivu ili kuweza kupata utaalamu pia kutumia utaalamu huo pindi watakapporejea kwenye shughuli zao.

Pamoja na hayo ameielekeza TBS kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa kushirikiana na watendaji waliopo katika halmashauri zetu nchini ili kurahisisha kufiikisha huduma kwa wananchi.

"Nazielekeza Halmashauri zote za Mkoa wa Lindi kuendelea kutoa ushirikiano kwa TBS ili kuwahudumia wananchi wetu kwa ufanisi na kwa haraka". Amesema RC Tereck.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: