Na Lucas Myovela_ Arusha.

Pichani ni Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini Mhe, Sophia Mjema Akiongea na viongozi mbali mbali pamoja na wadau wa Sekta ya Afya katika ukumbi wa Mkoa Jijini Arusha.

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella, ametoa muda wa siku tatu kwa wakuu wa wilaya yake kuitisha Vikao vya kamati za msingi za afya ngazi za Kata ili kuelimisha wananchi na kuwahamasisha ili washiriki katika zoezi la uchomaji wa chanjo ya Uviko 19.

Hayo yameelezwa na kaimu Mkuu wa Mkoa huo, Mhe,Sophia Mjema, alipokuwa akifungua kikao cha kamati ya afya ya msingi ya Mkoa kikao hicho chenye lengo la kutoa elimu muhimu ya Ugonjwa wa Uviko 19 pamoja na chanjo ya Uviko 19 ambapo mpango muhimu ni kuharakisha utoaji wa Chanjo hiyo ili kukabiliana na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya Uviko 19, Ambapo Mkutano huo umewshirikisha wadau mbali mbali latila sekta ya Afya pamoja na viongozi wa Serikali, Mila pamoja na dini.

"Kasi kubwa inayoendelea kuchukuliwa juu ya utoaji wa elimu ya Uviko 19 hasa katika wimbi hili la tatu ni chachu kubwa ya mapambano dhidi ya ugonjwa huu, Tahadhari kubwa tunazo chukua dhidi ya kujikinga ikiwemo utoaji wa chanjo ili kujikinga na kirusi hatari ambacho kimesababishia majanga taifa letu na dunia kwa ujumla wake" Alieleza Dc Mjema.

"Katika Mkoa wa Arusha uzinduzi wa uchomaji chanjo ulifanyika 8.8.2021 na tulizindua tukowa na vituo 20 na mpaka sasa tunanvyo vituo 120  ambavyo vinatumika kutoa chanjobya Uviko 19.

"Niwaombe vijana kwenda kupata chanjo ya Uviko 19 maana maradhai haya sio ya wazee  kama inavyosemekana huko mitaani na ikimbukwe chanjo hii ni salama na inatolewa kwa hiyari tena ni bure, Tuendelee kuhamasishana maana ukipata chanjo hupunguza maambukizi na kupunguza makali ya ugonjwa huu pindi utakapo ugua". Aliongeza Dc Mjema.

Kwa upande wake Mkurunzi Mkazi wa shirika la EGPAF, Bi, Sajida Kimambo, Ameahidi kuendelea kushriikiana na serikali Katika mapambano dhidi  ya maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 ilii kupunguza kasi ya maambukizi ya Uviko 19 ili kuweza kufikia malengo.

"Maambukizi ya ugonjwa huo bado yapo juu hivyo inahitajika nguvu ya pamoja katika kukabiliana na ugonjwa huo, kulingana na kauli mbinu ya  afya isemayo afya bora ni mtaji mapambano ya Uviko -19 ni wajibu wetu tujumuike kuchanja kwa kuwa chanjo ni salama". Ameeleza Bi Kimambo.

Aidha Kimambo aliezakuwa kuna changamoto ya kupokelewa  kwa chanjo hiyo kwa baadhi ya wahudumu wa afya na wananchi hivyo shirika hilo litaendelea kushirikiana na serikali katika kutoa elimu sahihi waweze kupata chanjo hiyo ili wajikinge na maambukizi ya ugonjwa huo wa Uviko -19.

Kwa upande wake Mratibu wa chanjo ya Uviko -19 Mkoa wa Arusha, Wilson Lokindalaki,amesema Jiji la Arusha ndilo linaongoza kwa kutoa chanjo nyingi ambapo limefikia asilimia 87% likifuatiwa na halmashauri ya Meru ambayo imefikia asilimia 79% huku wilaya zingine zimefikia asilimia 30 hivyo muitikio bado ni mdogo.

"Takwimu ya Mkoa wetu wa Arusha imefikia asilimia 62% huku asilimia 38% ya chanjo bado haijatumika hivyo juhudi Zaidi zinahitajika ili kuwezesha kufikia asimilia 100%, kwa sasa vituo vya utoaji wa chanjo vimeongezeka kutoka vituo 20 hadi kufikia vituo 120 na chqnjo zitatolewa mda wote". Alieleza Wilson.

Awali Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Daktari Sylivia Mamkwe, amesema kwamba Viongozi  wanalo jukumu kubwa la kwenda kuelimisha na kuhamasisha wananchi kwenye maeneo yao ili kutekeleza mpango wa Wizara ya Afya wa kutolewa chanjo hiyo ya Uviko 19.

"Wagonjwa wa Uviko -19 hawaonyeshi dalili zozote kama mwanzo sasa wagonjwa wanapofika hospitalini wanapofanyiwa vipimo inabainika mapafu yao yameshaathirika na wana ugonjwa wa ammonia kali hivyo chanjo itasaidia kuokoa Maisha ya wananchi". Alieleza Dkt Mamkwe.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ua Monduli Mhe, Frank Mwaisumbe ameeleza kwamba wao kama viongozi watazidi kushirikiana na wadau wa Afya hasa katika kutoa elimu pamoja na chanjo katika jamii wanazo ziongoza hasa jamii za ufugani ili kuendelea kufanya vizuri zaidi katika juhudi za kukabiliana na maambukizi ya Uviko 19.

"Kwa pamoja niwashukuru viongozi wa Serikali pamoja Waandishi wa Habari hasa wa Mkoa wetu wa Arusha kiukweli walikuwa mstari wambele katika kuelimisha wananchi juu ya namna ya kujikinga na ugonjwa wa Uviko 19, nasisi kama viongozi ngazi ya Wilaya nijuku letu kwenda kubimiza zaidi ili elimu ifike zaidi kwa wananchi".Alisema Dc Mwaisumbe.
Share To:

Lucas Myovela

Post A Comment: