Thursday, 23 September 2021

NIC YATOA MSAADA WA VITI NA MEZA 200 KWA SHULE ZA SEKONDARI TATU ZA MANISPAA YA KIGAMBONIMkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa akikata utepe baada ya kupokea msaada wa viti na meza kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwaajili ya wanafunzi katika baadhi ya shule katika wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa akingumza mara baada ya kupokea msaada wa viti na meza kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwaajili ya wanafunzi katika baadhi ya shule katika wilaya hiyo.


Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo Karimu Meshack akizungumza mara baada ya kukabidhi meza na viti 200 katika shule za Sekondari zilizopo wilayani kigamboni kwaajili ya wanafunzi.Katibu Tawala wa Manispaa ya Kigamboni Bi.Dalmia Mikaya akizungumza baada ya kupokea msaada wa viti na meza kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwaajili ya wanafunzi katika baadhi ya shule katika wilaya hiyo.


Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa akingumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Aboud Jumbe mara baada ya kupokea msaada wa viti na meza kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC) kwaajili ya wanafunzi katika baadhi ya shule katika wilaya hiyo.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Aboud Jumbe Bi.Rose Mkono akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa viti na meza kutoka Shirika la Bima la Taifa (NIC). NIC limekabidhi viti na meza 200 kkwa shule za sekondari Kigamboni.


(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)


*****************************


SHIRIKA La Bima la Taifa (NIC,) limetoa msaada wa viti na meza na viti 200 vyenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa shule tatu za Sekondari za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni ikiwa ni sehemu ya kutekeleza sera ya shirika hilo ya kurudisha kwa jamii pamoja na kushirikiana na Serikali katika kuboresha sekta ya mbalimbali muhimu zinazoigusa jamii ikiwemo elimu kwa shule za msingi na sekondari pamoja na afya.


Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Mhe.Fatma Nyangasa amesema NIC imekuwa ikishiriki shughuli mbalimbali za kijamii na kwa kutoa msaada huo wa viti na meza 200 imewezesha kutatua kabisa changamoto ya viti na meza kwa wanafunzi wa kidato cha tano wa shule za Aboud Jumbe na sekondari za Kisarawe II na Minanzini.


"Taasisi, jamii na wadau wa elimu tunawaomba wafuate nyayo za NIC kwa kushiriki katika kusaidia miundombinu rafiki ya elimu ili kuwawezesha wanafunzi katika Halmashauri yetu kusoma katika mazingira wezeshi ili waweze kufanya vyema katika mitihani yao ya kuhitimu.....Nawaomba NIC mnifikishie salamu za shukrani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa- NIC, Dkt. Elirehema Doniye tutarudi tena tena tunaomba mtupokee.'' Amesema Nyangasa.


Aidha amewataka walimu na wanafunzi wa shule hizo kutunza rasilimali hizo kwa manufaa ya waliopo na watakaofika ili kuwapa moyo zaidi wanaotoa misaada hiyo kuendeleakushiriki katika kuboresha sekta hiyo muhimu ya elimu pamoja na kuwataka wanafunzi hao kuzingatia masomo na kuendelea kupeperusha vyema bendera ya Manispaa hiyo kitaaluma.


Akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa NIC, Meneja Mawasiliano wa Shirika hilo Karimu Meshack amesema wamekuwa wakitekeleza sera ya shirika hilo la kurudisha kwa jamii pamoja na sera ya Serikali na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM,) katika kuunga mkono jitihada katika sekta ya elimu kwa shule za msingi na sekondari.


Amesema kuwa NIC imefarijika kwa kutatua changamoto ya viti na meza kwa wanafunzi wa kidato cha tano ya Aboud Jumbe na kunufaisha shule tatu za Sekondari za Kisarawe II na Mianzini na kuahidi kuendeleza ushirikiano katika masuala yanayoigusa jamii wanayoihudumia.


Akitoa taarifa kwa niaba ya shule zilizonufaika na msaada huo mkuu wa shule ya Aboud Jumbe Rose Mkono amesema NIC walitoa shilingi milioni 20 zilizoelekezwa katika miundombinu ya viti na meza zoezi lililosimamiwa na ofisi ya Mkurugenzi na ofisi ya Mkuu wa Wilaya zoezi ambalo limeleta manufaa kwa wanafunzi wa shule hizo.


Amesema katika msaada huo wanafunzi 200 wamenufaika na msaada huu, thamani ya kila kiti na meza imegharimu shilingi laki moja na katika mgawanyo Sekondari ya Aboud Jumbe imepata viti na meza 110, Kisarawe II 40 na Minanzini 50 na kuwasilisha changamoto ya samani kwa walimu wa shule hiyo ambayo ilichukuliwa na Meneja Mawasiliano wa NIC kwa hatua zaidi.


Bi. Mkono ameishukuru NIC kwa kuona umuhimu wa kushiriki na kutoaa msaada kwa wwanafunzi wa shule hizo na kuiomba jamii, taasisi mbalimbali na wadau wa elimu kufuata nyayo za shirika hilo ili kuoboresha zaidi sekta ya elimu nchini kama Serikali ilivyodhamiria.

No comments:

Post a Comment