Na Mwandishi wetu ,Tanga


NAIBU Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) atembelea sekondari ya Lazoni iliyopo Kata ya Mhinduro, Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga na kuahidi shule hiyo kufikishiwa huduma ya maji.


Mkuu wa shule hiyo Bw. Deudatus Kapumila amesema shule hiyo haipati maji  licha ya uwepo wa miundombinu ya maji.


Amesema hali hiyo inahatarisha maisha ya watumishi wa shule wanapoenda kuchota maji mtoni, ikiwano kushambuliwa na mamba. 


Kufuatia hali hiyo  Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi ameelekeza RUWASA Wilaya ya Mkinga kufanyia kazi suala hilo ndani ya mwezi mmoja na kuhakikisha maji yanafika katika shule hiyo.


Mahundi ametumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi kuzingatia masomo yao  ili waweze kutimiza ndoto na malengo. 


Kufikisha huduma ya majisafi katika maeneo yanayohudumia jamii ni moja ya kipaumbele katika sekta ya maji hapa nchini. Sekondari ya Lazoni ilianzishwa zaidi ya miaka 26 iliyopita.


Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: