KIONGOZI  wa Mbio maalumu za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2021, Luteni Josephine Mwambashi ameridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji Mababu wilayani Kyela mkoani Mbeya na kuagiza mwishoni mwa mwezi huo mradi huo ukamilike na kutoa huduma kwa wananchi. 

Luteni Mwambashi ameyasema hayo jana mara baada ya Mwenge wa uhuru kutembelea mradi huo kwa lengo la kukagua utekelezaji wake.

 “Mradi huu ulipitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2019. Leo tulikuja kuangalia hatua iliyofikiwa na kujiridhisha iwapo unatekelezwa katika viwango vilivyokusudiwa tumeridhishwa na utekelezaji hivyo hadi mwishoni mwa mwezi huu mradi huu uwe umakamilika na wananchi wapate huduma ya maji.” amesema Luteni Mwambashi.

Aidha, kiongozi huyo amewataka wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya Maji ili isiharibiwe.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge kupitia viti maalumu wanawakle mkoa wa Mbeya amemhakikishia kiongozi  huyo kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati.

Amesema mradi huo ulikuwa na vituo  vitano vya kuchotea maji, Serikali chini ya Mheshimiwa Rais Samia iliongeza fedha kiasi cha shilingi milioni 207 ambazo zimewezesha kuongeza miundombinu ya mabomba,  tenki la kuhifadhia Maji pamoja na vituo vinne zaidi vya kuchotea Maji kutoka vitano vilivyokuwa katika bajeti ya awali.

Meneja wa Wakala wa Maji Vijijini Wilaya ya Kyera Mhandisi ,Tanu Deule amesema mradi huo unatarajia kuhudumia wakazi 5,121 kutoka vitongozi vitano vya kijiji cha Mababu ambapo gharama ya utekelezaji inatarajiwa kuwa zaidi ya shilingi  milioni 398.

Mwenge Maalumu wa Uhauru uko mkoani mbeya ulkitarajia kukamilisha mbio zake mkoani hapa Septemba 15 mwaka huu.

Share To:

Post A Comment: