September 21, 2021 Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson, amezungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwake Uzunguni na kuwaeleza kuhusu ujio wa mashindano ya ngoma za jadi yanayofahamika kama Tulia Traditional Dances Festival yanayotarajiwa kufanyika September 23-25 Jijini humo.


“Ndugu zangu nimewaita leo hii ili kuwaeleza kwamba kuanzia siku ya tarehe 23-25 mwezi huu wa tisa tutakuwa na tukio kubwa na la kihistoria ambalo kwa miaka minne mfululizo limekuwa likifanyikia katika Wilaya ya Rungwe na mwaka huu tumeamua kulileta ndani ya Jiji la Mbeya nalo si lingine bali ni Tulia Traditional Dances Festival” -Dkt. Tulia Ackson


“Haya ni mashindano ya ngoma za jadi ambayo yanazikutanisha tamaduni kutoka mikoa yote nchini ambapo washiriki wanashindanishwa uwezo wao na washindi wanapewa zawadi mbalimbali huku lengo kuu likiwa ni kuuenzi utamaduni wetu.” -Dkt. Tulia Ackson


“Nje na kutangaza utamaduni wetu lakini pia Tulia Traditional Dances Festival ni sehemu pia ya kutengeneza fursa za kipato kwa Wananchi mbalimbali ambao kwa kupitia mashindano hayo wataweza kufanya biashara zao na mambo mengineyo” -Dkt. Tulia Ackson


“Tamasha letu la mwaka huu litakuwa na utofauti kidogo kwasababu tunatumia sehemu hii kama fursa ya kiuchumi kwa Wananchi wetu lakini pia kama sehemu ya watu wengine wakiweno wasanii wetu kujifunza, mtoto wetu Rayvanny naye atakuwepo siku ya ufunguzi kwa ajili ya kutumbuiza na hata kuzungumza na baadhi ya wasanii wetu wa hapa Mbeya kwa lengo la kuwaonesha njia nzuri ya kuyafikia mafanikio”- -Dkt. Tulia Ackson


“Kama nilivyosema kwamba tamasha hili linakusudia kuleta fursa nyingi ikiwemo za utalii katika mikoa yetu ya Nyanja za juu kusini, tunatarajia kuwa na baadhi ya Viongozi wa Serikali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii pamoja na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo hivyo basi niwaombe watu wajitokeze kwa wingi katika shindano letu”-Dkt. Tulia Ackson

Share To:

Post A Comment: