Friday, 24 September 2021

Dc Mbogwe aipongeza Tume ya Madini kwa kutoa Leseni za MadiniMkuu wa Wilaya ya Mbogwe Eng. Charles F. Kabeho ameipongeza Tume ya Madini kwa kutoa leseni nyingi za Madini kwa Wachimbaji wadogo wadogo Katika Wilaya yake 


Ameyasema hayo leo tarehe 24.09.2021 alipotembelea Banda la Tume ya Madini kwenye Maonesho ya Nne ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini  katika Viwanja vya Maonesho Bombambili EPZ Mkoani Geita.


“Niwashukuru Tume ya Madini kwa kazi kubwa mnazozifanya, mmeweza kuwapatia Wachimbaji wadog wadog Leseni za kutosha Katika Wilaya yangu  na kuwawezesha kuchimba Katika maeneo yao.”


Ametoa wito kwa Wachimbaji kutembelea Banda la Tume ya Madini kujifunza namna ya kujisajili leseni za Madini kwa njia ya kimtandao.


“Wachimbaji wadogo mtembelee Banda la Tume muweze kujifunza kanuni, Sheria na taratibu ili ziweze kuwaongoza Katika shughuli za Uchimbaji alimalizia kusema Mkuu wa Mkoa.”```

No comments:

Post a Comment