RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.

Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) Dk.Bwire Chirangi akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu  wa 84 wa mwaka  wa maaadaktari hao uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma .

Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.

RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,akipokea kasha la tair la gari kwa ajili ya kupandika kwenye gari lake ujumbe uliopo katika kasha hilo mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.

RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA) uliofanyika leo September 6,2021 Jijini Dodoma.

.........................................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

RAIS wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ,Askofu Gervas Nyaisonga amewataka  Madaktari nchini   kuwa na huruma  pamoja na kujiepusha na  vitendo vya rushwa wakati wa kuwahudumia  wagonjwa wanaofika kupata huduma za afya kwenye maeneo yao.

Kauli hiyo ameitoa leo September 6,2021 jijini Dodoma wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 84 wa mwaka wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania (TCMA),Askofu Nyaisonga amewataka Madaktari hao kuwa na huruma kwa wagonjwa na kuejiepusha na vitendo vya rushwa wakati wa kuwahudumia wagonjwa kwenye maeneo yao.

“Hapa juzi niliona clipu ya video na kuelezwa kuwa kunadaktari kamshona mgonjwa lakini  inadaiwa kuwa baada ya kukosa fedha alimfumua huo mgonjwa,bahati nzuri sio wa hospitali zetu za diniya Kikristo,hivyo tuwe na huruma kwanza bila kujali masilahi ya fedha ”amesema Askofu Nyaisonga 

Askofu Nyaisonga amesema  kazi ya kuwahudumia wagonjwa ni  ya wito,hivyo wanapaswa kufanyakazi kwa moyo  wa kuthamini maisha ya binadamu na kujituma  bila kushawishika au kuwa na tamaa ya kujinufaisha .

Amesema  madaktari hao  wamepewa dhamana ya kutunza afya za watu hivyo wanatakiwa kuzingatia maadili ya kazi yao na wajitume katika kuokoa  maisha ya watu

Amewataka  kujiepusha na mienendo inayochafua maadili ya udakitari na kuchafua Kanisa  kwa sababu kazi zao inakiapo na ndani ya kiapo hicho huishi kusema Mungu anisaidie maana yake ni kazi muhimu sana  kila siku .

Askofu Nyaisonga ameishukuru serikali  kwa kuendelea kuruhusu na kushirikiana na mashirika ya dini zote nchini katika kuanzisha na kutoa huduma za kijamii hasa afya.

“Nawashukuru  madaktari nchini kwa jinsi wanavyofanyakazi katika mazingira magumu hasa tangu ulipoingia ugonjwa wa homa ya Korona (UVIKO 19) pamoja na kukabiliwa na tatizo la rasilimali fedha lakini wamejitoa kuwasaidia wagonjwa,”amesema.

Amewataka  madakitari hao kuwa viongozi wa Makanisa ya Kikristo Tanzania wataendelea kushirikiana na TCMA katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi kwani taifa lisilokuwa na afya haliwezi kuwa imara  na kupata maendeleo

Naye,Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania ,Dk Bwire  Chirangi amesema mkutano huo wa 84 wa mwaka unajumuisha madaktari zaidi ya 300 kutoka vituo,zahanati na hospitali za makanisa yote nchini.

Amesema  kuwa mashirika hayo ya dini yanachangia kwa kiwango kikubwa huduma za afya na ustawi wa jamii kuna hospitali 105 ambapo kati ya hizo 38 ni teule za Halmashauri  na 10 zimepewa  hadhi ya rufaa ya ngazi ya Mkoa .

Dk Chirangi amesema  mashirika hayo yanamiliki zahati 720 na vituo vya afya 100 kote nchini  na wanaendesha baadhi ya vyuo vya mafunzo ya wauuguzi na madaktari pamoja na vyuo vya kufundisha wataalamu wa ngazi mbalimbali.

Share To:

JOHN BUKUKU

Post A Comment: