Jane Edward, Arusha


Wizara ya viwanda na biashara imesema kuwa Ina mpango wa kuomba bunge liridhie Tanzania kujiunga na mkataba wa biashara huru ukanda wa Afrika ambapo amesema kuwa viwanda vyetu hapa nchini vinahitaji ushindani mkubwa ndani ya dunia na Afrika kwa ujumla.


Hayo yamesema na waziri wa viwanda na biashara Profesa Kitila Mkumbo, wakati akiongea na kamati ya Bunge ya bajeti walipotembelea kiwanda Cha Ato Z ambapo alisema kuwa Tanzania ikisaini mkataba huo utasaidia kufungua masoko katika nchi 54 za Afrika.


“Tanzania imejiunga na jumuiya mbalimbali za kiuchumi EAC na SADIC ambapo kwa kusain mkataba huo itasaidia viwanda vyetu kujipanga zaidi katika kushindana na kiwanda hiki pamoja na vingine uzalishaji wao ni wa kimataifa na bidhaa zinakidhi viwango vya kimataifa,”Alisema Profesa Mkumbo.


Aidha Profesa Mkumbo amesema kuhusiana na kamati ya Bunge ya bajeti mojawapo ya mambo watakaosaidia Ni pamoja na mambo ya kodi ambapo watasaidia kujenga hoja kuishauri wizara ya fedha kuona kwamba Kodi wanazoziweka ziwe Ni Kodi ambazo zinachochea uzalishaji katika viwanda pamoja na kuweza kushindana katika soko la ndani ya nchi na ukanda wa Afrika.


Kwa upande wake meneja masoko ya nje kutoka kiwanda Cha A to Z Silvester Kazi alisema kuwa changamoto kubwa zaidi inayokabili ni marejesho ya VAT ambayo yamechelewa sana ambapo wameiomba kamati iweze kusaidia fedha hizo ziweze kutoka kwa wakati ili waweze kuwekeza na kuongeza uzalishaji zaidi.


Alisema kuwa changamoto nyingine ni ongezeko la kodi kwenye nyuzi za pamba kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 25 ambapo wameiomba serikali kurudisha kwenye kiwango cha awali kwani kuna mikataba ya mauzo ambayo walishaingia na haiwezekani kuongeza Bei ya bidhaa hizo tena, hali inayohatarisha ustawi wa kiwanda kutokana na kutarajia kupata hasara.


Naye mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya bajeti Daniel Baran alisema kuwa wamesikia changamoto hizo na Kama kamati wamezichukua ili kwenda kushirikiana na serikali kuutafuta ufumbuzi kwani kiwanda hicho Ni moja kati ya viwanda vinavyofanya vizuri katika ulipaji wa kodi ambapo kwa mwaka wanalipa zaidi ya bilioni 17.


Alisema pamoja na ulipaji wa kodi pia kiwanda kimeajiri zaidi ya watanzania 800 hivyo kamati imejione uhalisia wa bidhaa wanazozizalisha ambapo wameelekeza uongozi wa kiwanda hicho kuwaandikia changamoto hizo rasmi ili waweze kuzichambua na kuona katika bajeti ijayo Ni namna gani serikali itaingilia kati na kubadilisha viwango hivyo vya kodi.


MWISHO....

Share To:

Post A Comment: