Kundi
la wadau wa maendeleo Mkoa wa Mara wanaoishi na kufanya kazi sehemu
mbali mbali hapa nchini (Mara Investors) limekabidhi jengo kwa ajili ya
ofisi ya Serikali ya Mtaa ili kusaidia huduma za kiutawala kwa wakazi
wa mtaa wa Serengeti Kata ya Nyatwali Bunda mjini.
Jengo
hilo lenye thamani ya Shilingi 15.5 limejengwa kwa msaada wa wadau wa
maendeleo wa mkoa Mara ikiwa ni Pamoja ,Dkt. Amon Manyama, Dkt.
Sebastian Ndege na Wakili Deus Mgengeli.
Wadau
hao wamejitolea kujenga ofisi hiyo ili kusaidia upatikanaji wa huduma
za Kiserikali katika ngazi ya mtaa kutokana na mahitaji yanayokuwepo kwa
Muda mrefu.Pia linatarajiwa kuwa kituo cha taarifa mbalimbali za
kitalii na uwekezaji Katika eneo la Nyatwali,Bunda.
Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi jengo hilo, Agosti 8,2021 Mkuu
wa Wilaya ya Bunda Joshua Nasari aliwashuru wafadhili hao na kuwataka
wakazi wa Bunda kupokea kwa mikono miwili ofisi hiyo na kujipanga kwa
kumalizia kuongezea kile kilichopungua kwenye ofisi hiyo.
Nasari
alisema ofisi hiyo itakuwa ni msaada mkubwa kwa kuwa Pamoja na kutoa
huduma za kiserikali kwa wananchi wa eneo hilo, pia itatoa huduma ya
taarifa za utalii hususani katika ukanda wa Magrabi mwa Serengeti.
Mkuu
huyo wa wilaya aliwashukuru Mara Investors kwa kujitolea kujenga ofisi
hiyo na kuwataka wadau wengine kujitokeza katika kusaidia jamii
kupambana na changamoto mbali mbali ili kuweza kupata maendeleo.
"Sekta
binafsi ni wadau wetu katika maendeleo ya nchi kwa ujumla,Serikali
pekee haitoweza kufanikisha.Na nyie wananchi muunge mkono juhudi za
serikali kwa kuchapa kazi,kupiga vita uzembe na tabia za umbea na
uzururaji'',alisema Nassari.
Pamoja
na kushiriki kuzindua ofisi hiyo Nassari hiyo alipata fursa ya kupanda
miti kadhaa ikiwa ni ni sehemu ya uhamasishaji wa kutunza mazingira
wilayani humo.
Kwa
upande wake, Dkt. Amon Manyama, mmoja wafadhili walichangia ujenzi
,alisema yeye Pamoja na wenzake wamejipanga kwa ajili ya kusaidia
kufikisha huduma ya maji na Umeme pamoja na miundombinu ya taa za
kutumia umeme wa jua (solar) ili kuimarisha na kusaidia shughuli za
kiuchumi na kijamii katika eneo la Ndabaka Centre.
Naye
mwekezaji kutoka Jembe Group Dkt. Sebastian Ndege aliiomba serikali
kuendelea kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya kusaidia uwekezaji wenye
tija unaofanywa na sekta binafsi.Aidha Dr Ndege aliahidi kuendelea
kusaidia jitihada mbali mbali za kimaendeleo katika mtaa wa Serengeti
kwa kufadhili Ujenzi gati ya Maji safi na Salama na Choo cha Kisasa kwa
ajili ya wageni na watalii wanaopita eneo hilo.Aidha amewataka uongozi
wa Wilaya kunadili matumizi ya Soko lililojengwa hapo na kuwa
gofu,litumike kama soko la kitalii ambapo litatoa ajira kwa vujana na
kina mama wa Mtaa huo.
Mwekezaji
mwingine kutoka Mara Investors Wakili Deogratius Mgengeli aliiomba
serikali kushughulikia kero ya umiliki wa ardhi kupitia Hati za kimila
ili ziweze kutumika kupata mikopo ya uwekezaji katika eneo hilo.
Post A Comment: