Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. RoidaAndusamile (kushoto) akimkabidhi cheti cha Usajili wa Jina la Biashara Bw. Ibrahim Kahamba Shekhan (kulia) mara baada ya usajili wa papo kwa hapo katika banda la BRELA la Maonesho ya Sabasaba kwenye Viwanja vya Maonesho vya Mwalimu. Julius Nyerere, Jijini Dar esSalaam.

AfisaBiashara Bw. Paul Peter akitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA kwa Wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Jikomboe iliyopo Chato, Geita walipofika katika banda la taasisi hiyo kwenye Tamasha la kuhamasisha Utalii na Maonesho ya biashara Agosti15, 2021.


Na Mwandishi Wetu


WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imejipanga kuwafikia afanyabiashara  katika Mikoa yao kuwapa elimu ya kurasimisha biashara pamoja na kuwafanyia usajili wa papo kwa papo.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 18, 2021 na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano BRELA, Bi. Roida Andusamile alipokuwa akizungumza naWatendaji wa kitengo hicho juu ya shughuli za uhamasishaji na maonesho.

“Kwa mwaka wa fedha unaoanzia Julai 2021 na kuishia Juni 2022, BRELA itahakikisha kwamba elimu kuhusu sajili za  kibiasharainawafikia wadau wote ili waweze kuhamasika kuingia katika biashara kwa namna sahihi.

Siku zote tumekuwa tukiwapa elimu wadau wetu kwamba, ili kuanza biashara kwa usahihi BRELA ndio lango la kuingilia, unafanyausajili kwanza kuhakikisha kwamba jina la biashara au Kampuni yako upo peke yako unalitumia kisha mambo mengine yafuate” amesema Bi. Andusamile.

Katika hatua nyingine ameeleza kuwa maandalizi ya kufanya shughuli za uhamasishaji zipo katika hatua za mwisho ambapo maafisa watatembea katika Mikoa mbalimbali kwa ajili ya kutoaelimu kwa umma.

Imeelezwa kwamba elimu itakayotolewa katika shughuli hizo za uhamasishaji na elimu kwa umma ni pamoja na Usajili wa Kampuni, Majina ya biashara, Jinsi ya kupata Leseni ya Kiwanda, Leseni ya Biashara  kundi A na Hataza.

Bi. Andusamile amefafanua kwamba utekelezaji wa shughuli hizo ni kuitikia wito wa wadau wa BRELA ambaowamekuwawakijitokezakwawingi pale taasisiinaposhirikikatikamaoneshombalimbali.

“Tunaposhiriki katika maonesho wadau wengi wanajitokeza kupata usaidizi katika urasimishaji wa biashara, watu wengi walijitokeza katika Maoneshoya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es salaam (DITF), Maoneshoya 16 ya Elimu ya Juu, SayansinaTeknolojia, Maonesho ya kuhamasisha Utalii na biashara na mengine mengi ambayo BRELA imeshiriki, kupitia kwa washiriki tumepata maoni yao na sasa tunaelekea kuyatekeleza” ameeleza Bi. Andusamile.

BRELA ilianzishwa chini ya Sheria za Wakala wa Serikali No. 30 yaMwaka 1997 na kuzinduliwa rasmi tarehe 03 Disemba, 1999 chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara. 

Jukumu la msingi ni kusimamia ufanyikaji wa biashara nchini kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo kwa lengo la kuweka mazingira mazuri ya kibiashara.



Share To:

Post A Comment: