Thursday, 15 July 2021

TARURA MAKAO MAKUU ACHENI KUKAA OFISININa. Angela Msimbira KATAVI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewaagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA)  Mkao Makuu kuacha kukaa  0fisini waende kwenye maeneo ya vijijini  ili kuona  changamoto na ubora wa barabara.


Ametoa agizo hilo leo  alipotembelea na kukagua  utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata ya Katuna, Halmashauri ya Wilaya Tanganyika Mkoani Katavi  kwa lengo la kujua changamoto zinazozikabili Halmashauri  zilizopo pembezoni.


Waziri Ummy alifafanua kuwa TARURA makao makuu wanatakiwa kutoka ofisini watembelee vijijini kujua maeneo ambayo yanachangamoto ya miundombinu ili kuweza kutoa vipaombele zaidi wakati wa kupanga bajeti za utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara nchini.


“Haiwezekani TARURA mkakaa ofisini wakati matatizo mengi yanapatikana kwa wananchi hasa wale wanaokaa pembezoni, nawaagiza kuanzia sasa waache kukaa ofisini watoke na kwenda ‘site’ kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi hasa katika maeneo ya vijijini,” alisisitiza Waziri Ummy 


Alisema kwa sasa Serikali imejiwekea mkakati wa kuhakikisha  inatatua changamoto za miundombinu ya barabara vijijini.

 Alielieleza kuwa haiwezekani kukaa ofisini na kugawa fedha  bila kujua changamoto  za maeneo husika  kwa sababu haki itakuwa  haitendeki kwa baadhi ya Mikoa ambayo mtandao wao wa barabara ni mkubwa. 


“Tumegundua kuwa kuna baadhi ya Halmashauri atuzitendei haki kwa kuwa mtandao wa barabara za TARURA haufiki hata kilometa 200 lakini kuna maeneo ambapo mtandao wao wa barabara ni zaidi ya kilometa 1900. Sasa unaposema Halmashauri zote zipate sawa hii si haki. Tunaenda kuzifumua bajeti za maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa barabara ili kuziwezesha Halmashauri ambazo zinachangamoto kubwa” alisisitiza Waziri Ummy 


Naye Mbunge wa Mpanda Vijijini Mhe Selemani Kakoso ameiomba Serikali  kusaidia kujenga barabara ya kutoka Sibwesa – Kaduma  yenye urefu wa kilometa 25 ambayo ipo katika mtandao wa TARURA.

No comments:

Post a Comment