Friday, 30 July 2021

Tanesco mkoani Arusha yafanya ukaguzi na kubaini wizi wa umeme .

 


Jane Edward, MsumbaNewsShirika la umeme Tanzania Tanesco mkoani Arusha ,limefanya ukaguzi katika maeneo ya kata ya Murieti Mkoani Arusha na kubaini nguzo za umeme zaidi ya 12 zilizotumika kuunganisha umeme kwa njia za wizi.


Akizungumza wakati wa ukaguzi huo wa kubaini maeneo korofi yanayo hujumu miundombinu ya shirika hilo,  Afisa usalama wa shirika hilo John Chirare, amesema kuwa, wananchi wanatumia vishoka kuhujumu miundombinu hali inayosababisha uwepo wa  nguzo zisizofata taratibu na  mwisho wa siku kuhatarisha maisha ya wananchi.


Ameongeza kuwa serikali kupitia shirika hilo ipo imara kulinda miundombinu yake na kwamba nguzo hizo zilizopatikana zitatumika kama kielelezo katika kufungua kesi dhidi ya wahujumu wa shirika hilo.


"Nawataka wananchi kuhakikisha kuwa wanafuata sheria na taratibu zilizowekwa kwani kutumia vishoka kujiunganishia umeme bila kufuata utaratibu ni kinyume cha sheria na shirika halitamuonea  haya mtu yeyote anakayebainika kufanya hivyo" amesema Chirare.


Baadhi ya wananchi ,Hawa Said,amesema kuwa uwepo wa vishoka hao wanasababishwa na shirika hilo kutokupeleka huduma ya umeme kwa haraka kwa wananchi hasa maeneo yaliyopo pembezoni mwa mji.


"Sasa sisi tuna uhitaji wa umeme na tunaona wenzetu wana umeme  unajikuta umefanya hivyo ili kupata umeme kwa haraka,hivyo tunaiomba tanesco  kuharakisha miundombinu ya umeme  kwa haraka kwa wananchi ili kuondoa hii adha hiyo "amesema Hawa.


Hata hivyo shirika hilo limewataka wananchi kukaa kwa utulivu na kusubiri mradi wa upachikwaji wa nguzo hizo kwa ajili ya matumizi ya umeme na sio kutumia vishoka kuharibu miundombinu ya shirika hilo hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watakaobainika.


Mwisho.....

No comments:

Post a Comment