Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akionesha umahiri kwa kushona nguo wakati alipotembelea chuo cha  ufundi na marekebisho kwa watu  wenye ulemavu cha Sabasaba (VTC) kilichopo Kata ya Utemini mjini hapa..

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akizungumza na wanafunzi wa chuo hicho.
Mkuu wa chuo hicho, Fatuma Malenga akizungumzia juu ya utekelezaji wa program ya kukuza ujuzi kwa vijana inayofadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima, akimsalimia kwa unyenyekevu mkubwa mmoja wa wanafunzi wa chuo hicho.
 


Na Dotto Mwaibale, Singida.


SERIKALI imetoa Sh.173.7 kwa ajili ya gharama ya mafunzo ya ufundi kwa vijana mkoani hapa.

Hayo yamesemwa jana na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Musa Sima wakati alipotembelea   chuo cha  ufundi na marekebisho kwa watu  wenye ulemavu cha Sabasaba (VTC) kilichopo Kata ya Utemini mjini hapa.

Akiwa chuoni hapo Sima aliweza kuzungumza na vijana 70 wanaopata elimu ya ufundi kwa miezi sita kwa ufadhili wa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu. 

Akizungumza na vijana hao Sima alisema akiwa bungeni alitoa hoja kuiomba Serikali kugharamia elimu ya ufundi ili kupata vijana wengi wenye ujuzi ambao wataweza kujitegemea hoja ambayo ilikubaliwa na matokeo yake ndio hayo mafunzo yanayotolewa kwa vijana hao kwa ufadhili wa Serikali. 

Mbali ya chuo hicho vijana wanaonufaika na masomo hayo ni wa Chuo cha VETA chenye wanafunzi 246 na FDC chenye wanafunzi 60.

Sima alitumia ziara hiyo katika vyuo hivyo kuwaomba vijana hao kuzingatia masomo yao hayo ya ufundi ambayo yatawasaidia kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa.

"Jambo kubwa ambalo napenda kuwahimiza someni kwa bidii kwani ufundi mnaojifunza utawasaidia kujiajiri na kuondoa dhana ya kutaka kuajiriwa," alisema Sima.

Mkuu wa chuo hicho, Fatma Malenga alisema hivi sasa wanafanya utekelezaji wa program ya kukuza ujuzi kwa vijana inayofadhiliwa na Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo vijana hao wapatao 70 wanajifunza fani za umeme, ushonaji nguo,mapambo,useremala,ujenzi na kupaka rangi. 

Wanafunzi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti walimshukuru mbunge huyo na kumpongeza Rais Samia Saluhu Hassan kwa kutoa fedha zinazowawezesha kupata mafunzo hayo.

Share To:

Post A Comment: