Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa TANESCO wilaya ya Kongwa Shaban Seif wakati akikagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa wakati wa ziara ya Waziri huyo iliyofanyika leo Julai 27,2021.

Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akizungumza na wananchi wa Mbande wakati wa ziara ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.

Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akimsikiliza Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge,Job Ndugai wakati akizungumza na wakazi wa Mbande wakati wa ziara ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani, ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.

Mwenyekiti wa kijiji cha Mbande Bw.Peter Chiumbe akitoa kero ya umeme kwa Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,wakati wa ziara ya kukagua eneo la kufunga AVR lililopo Mbande wilayani Kongwa ziara iliyofanyika leo Julai 27,2021.

Meneja wa TANESCO wilaya ya Kongwa Shaban Seif,akielezea hatua za ujenzi wa Kituo cha Kupooza umeme kilichopo Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa.

Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa mara baada ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O kinachotarajiwa kujengwa katika eneo hilo.

Diwani wa Kata ya Ugogoni Mhe.Elizabeth Lenjima,akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani,ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O kilichopo Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa iliyofanyika leo Julai 27,2021.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa wakimsikiliza Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati wa ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Machenje.

Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani ,akizungumza na wananchi wa Kibaigwa mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa iliyofanyika leo Julai 27,2021.

Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge,Job Ndugai,akizungumza wananchi wa Kibaigwa mara baada ya Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa leo Julai 27,2021.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza wananchi wa Kibaigwa mara baada ya Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa leo Julai 27,2021.

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Emmanuel,akizungumza wananchi wa Kibaigwa mara baada ya Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa leo Julai 27,2021.

Baadhi ya wananchi wa Kibaigwa wakimsikiliza Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani (hayupo pichani) wakati akizungumza nao kuhusu changamoto za umeme mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua eneo la ujenzi wa Kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O katika Kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wilayani Kongwa leo Julai 27,2021.

.....................................................................................

Na Alex Sonna,Kongwa

MRADI mkubwa wa kujenga kituo cha kupooza umeme cha Kilovolti 22O wenye thamani ya shilingi bilioni 41.2 unatarajiwa kuanza kujengwa Septemba mwaka huu Wilayani Kongwa ambao utasaidia upatikanaji wa uhakika wa umeme katika maeneo hayo.

Hayo yamesemwa leo Julai 27,2021 na Waziri wa Nishati,Dkt.Medard Kalemani wakati wa ziara ya kukagua eneo la Ujenzi wa kituo hicho kilichopo kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni amesema kuwa Mhe.Rais,Samia Suluhu Hassan amesikiliza kilio cha wakazi wa Kongwa

Amesema kutoka katika kituo cha kufufua umeme cha Zuzu mpaka Kongwa ni kilometa 122 hivyo ni mbali kiasi ambacho umeme umekuwa mdogo na Dodoma limekuwa Jiji.

“Kwa heshima yenu sasa Mheshimiwa Rais amesikia kilio chenu na ameelekeza tujenge kituo cha kufufua umeme tena umeme mkubwa wa KV 220.Nimekuja kutekeleza agizo la Serikali hili eneo mlilopendekeza tunawashukuru kwani tunaenda kutatua tatizo la umeme katika eneo hili nimekuja hapa kutatua hii kero,”amesema

Amesema katika Mji wa Kongwa kuna miradi minne inaendelea ambapo ni wa kuleta umeme kwenye vitongoji,kusambaza umeme katika maeneo ambayo yapo karibu sana mitaa kama Mbande,kuboresha miundombinu ya umeme pamoja na mradi mkubwa wa kujenga kituo cha kupooza umeme.

“Yote hayo yanaifanya Dodoma kuwa na umeme wa uhakikika kuliko maeneo mengine.Kwenye mradi wa kuboresha miundombinu Serikali imetoa bilioni 2.7 kwenye Jiji zima lakini asilimia takribani 70 inakuja katika Jimbo la Kongwa,”amesema Dkt.Kalemani

Amesema kituo hicho kitahudumia maeneo yote yaliyokuwa na changamoto ya umeme ikiwa ni pamoja na umeme kutokukatikakatika na watapata umeme wa uhakika.

“Niwaombe sana Wananchi mchangamkie fursa wewe kama unafuga tumia umeme kama unalima tumia umeme kwavile ninyi ni wafugaji wekeni umeme hadi kwenye mazizi kwa ajili ya usalama wa wanyama wenu,”amesema.

Vilevile,amesema Serikali italipa fidia kwa wote waliotoa maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupooza umeme ambapo ekari 130 zitalipwa na jumla ya shilingi milioni 63 zimetengwa kulipa fidia.

“Ukigushwa utalipwa inategemea eneo lako lina nini na shughuli za ujenzi zinaanza kuanzia tarehe 1 mwezi wa 9 ni matarajio yetu mwakani muda kama huu kituo kitakuwa kimekamlika gharama ni bilioni 41.2,”amesema.

Kuhusiana na upatikanaji wa umeme katika vitongozi,Wilayani Kongwa,Waziri Kalemani amesema ameenda na Mkandarasi na Jumatatu ya wiki ijayo umeme utaanza kuwaka.

“Napenda nitamke kwamba nimekuja na Mkandarasi huyu hapa sijaja mikono mitupu na Meneja kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo maana amepewa vitongoji vyote vikiwemo vitongoji vya Machenjeni hapa Ugogoni na hapa mna vitongoji vinne,Chungu,Tandika A,Tandika B na Chandama, kuanzia Jumatatu mnaanza kuwasha umeme na tutaweka umeme kwenye vitongoji vyetu,”amesisitiza Dkt.Kalemani

Aidha Dkt. Kalemani amemtaka mkandarasi kuziwekea umeme nyumba zote bila kujali uzuri wa nyumba huku akiwataka wananchi kulipa shilingi 27 kama Serikali ilivyoelekeza.

“Ombi langu aanze kuweka nyaya msijali kwamba ubaya wa nyumba mkandarasi wewe peleka umeme usiruke nyumba hata moja bei inaelewa ni 27,000 hamuwezi kushindwa wenyeviti simamieni hili tuna Mheshimiwa Spika kaishaleta fedha za kutosha tuna bilioni 47 kuwaletea umeme kwenye vitongoji vyote,”amesema.

Amesema katika Jimbo la Kongwa wamebakisha vijiji vinne katika vijiji 87 ambavyo bado havijafikiwa ambapo amedai baada ya kumaliza katika vijiji watahamia katika vitongoji.

Kwa upande wake,Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Spika wa Bunge,Job Ndugai amesema wakazi wa Jimbo la Kongwa wamekuwa wakilalamika kuhusu umeme kukatika mara kwa mara.

“Mmekuwa mkilalamika sana kwenye mitandao yenu umeme ukikatika tu watu wa Kibaingwa tayari hata watoto wadogo wanajua jinsi Tanesco ilivyomaarufu yaani umeme ukikatika tu utasikia Tanesco, hata kitoto cha miaka miwili kinajua Tanesco kwanza kabla ya shirika lolote.

Spika Ndugai amesema lazima Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liondolewe katika sifa hiyo ambayo sio nzuri.

Naye,Kaimu Meneja wa Tanesco Mkoa wa Dodoma,Mhandisi Donasiano Shamba amesema ujenzi wa kituo cha Gridi cha 2x40MVA ,220 -33Kv Narco ambacho kitahusisha ujenzi wa laini ya msongo wa Kilovolti 220 kutoka Zuzu mpaka Narco Kongwa kwenye kijiji cha Machenje Kata ya Ugogoni wenye urefu wa km 122.

Amesema Tanesco wameishapata eneo lenye ukubwa ekari 130 ambapo zoezi la uthaminishaji kwa ajili ya fidia ya ardhi na mali limekamilika ambapo wananchi 38 watafidiwa kupisha eneo hilo la mradi.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: