Friday, 23 July 2021

RC TABORA KUUNDA TIMU YA KUSHIRIKIANA NA TRC KUFUFUA KARAKANA YA SAMANI

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (kushoto) akisisitiza jambo leo wakati ziara yake ya kujitambulisha na kukagua shughuli mbalimbali za Shirika la Reli Tanzania(TRC) Kanda ya Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (katikati) akiwa katika picha ya pamoja leo na baadhi ya Watendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Kanda ya Tabora na watumishi wa Chuo cha Teknolojia ya Reli cha Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (katikati) akitoa majumuisho ya ziara yake leo kwa baadhi ya watendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Kanda ya Tabora na watumishi wa Chuo cha Teknolojia ya Reli cha Tabora.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (mwenye usungi) akipata maelezo leo kutoka kwa Mkaguzi wa Kazi wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Kanda ya Tabora John Erasto jinsi mitambo mbalimbali iliyopo katika Karakana ya Rufita Mjini Tabora ambavyo bado ni mizima licha ya Karakana hiyo kutofanyakazi.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani (mwenye ushungi) akipata maelezo leo kutoka kwa Mhandisi Mitambo wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Kanda ya Tabora Rudolf Ngalason jinsi ya ukarabati wa vichwa vya treni unavyofanyika katika Karakana ya Reli iliyopo eneo la Cheyo mjini Tabora.

*************************

NA TIGANYA VINCENTMKUU wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema Wataunda Timu itakayoshirikiano na Shirika la Reli Tanzania na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ili kuhakikisha wanafufua karakana kumbwa ya mjini Tabora.

Alisema Karakana hiyo amabyo mitambo yake mingi bado inafanya kazi ni fursa kubwa kwa ujenzi wa uchumi wa Mkoa wa Tabora na uboreshaji wa Shirika la Reli la Tanzania(TRC)Dkt. Batilda ametoa kauli hiyo leo baada ya kumaliza ziara yake ya kujitambulisha na kukagua shughuli mbalimbali za Shirika la Reli Tanzania(TRC) Kanda ya Tabora.

“Hii mimi ninaiona kuwa ni fursa kwetu Tabora …tutaunda timu ambayo itashirikiana na wenzetu wa TRC na Wizara husika katika kuhakikisha inarejea katika utendaji wake wa awali ikiwe wa kupasua magogo makubwa, kutengeneza samani na kuweka urembo kwenye samani kwa ajili ya kuongeza mapato ya Mkoa wetu” alisisitiza.Amesema kufufuliwa kwa Karakana hiyo kutasaidia kuongeza fursa ya mapato kutokana na bidhaa mbalimbali ambazo zitazalishwa kwa kuwa kuna mitambo mikubwa ambayo inaweza kufanya kazi nyingi kwa muda mfupi na kutoa ajira kwa watu wengi.Aidha Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka Watendaji wa TRC Kanda ya Tabora kutumia njia hiyo ambayo ni Kitovu cha Usafishaji wa Reli kwa ajili ya kutoa fursa kwa wananchi wengi kutangaza bidhaa kama vile asali na mchele kwa wageni wa ndani na nje ya Nchi wanaotumia usafiri huo.


Alisema hatua itasaidia kuboresha mapato ya wananchi na uchumi wa Mkoa na hata mazingira ya Shirika kwa upande wa Tabora.

“Moja ya kitambulisho ya Tabora ni asali ni vema mkaweka mazingira wezeshi kwa wakazi wa Tabora kunufaika na njia hiyo kwa kuuza bidhaa za asili za aina mbaliambali badala ya kuuza soda na maji pekee” alisisitiza.

Kwa upande wa Chuo cha Teknolojia ya Reli(TIRTEC) , Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka kukitangaza zaidi ndani na nje ya Nchi ili kiweze kuongeza idadi ya wanachuo kinaodahili hivi sasa kutoka 288 hadi zaidi ya 400.

Alisema hatua hiyo ni lazima iendelea na kuongeza kozi wanazofundisha ikiwemo kuwa na asatashahada, stashahada na Shahada katika masomo yayohusiana na usafishaji wa Reli.

Dkt. Batilda alisema hali hiyo itawawezesha wahitimu kuwa na uwezo wa kuendesha Reli Treni ya Mwendo pindi itakapokuwa imekamilika.Meneja wa Usafirisahaji Kanda ya Tabora John Mamuya alisema wanatoa fursa kwa Wajasiriamali kufanyabiashara kwa wale wanaozigatia Sheria na taratibu.

No comments:

Post a Comment