Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela Akizungumza katika Mahafali ya Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu yaliyofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa.

Mwenyekiti wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha Baraka Solomoni, akifungua mahafali ya Wanafunzi wa vyuo na vyuo vikuu UVCCM, yaliyofanyikia jana katika Ukumbi wa Ccm Mkoa.

 Kaimu Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Uvccm Mkoa wa Arusha, Ibrahimu Kijanga akitoa maelezo kuhusu mahafali ya Wanafunzi wa vyuo hivyo.

Katibu wa Vyuo na Vyuo Vikuu Mkoa wa Arusha Wema David Somba akimsikiliza kwa makini mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa MNEC Annagatha Msuyaakizungumza na wahitimu.











Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amewataka wahadhiri wa vyuo vikuu kubadilisha mwelekeo wa vijana wa vyuo vikuu ili waweze kuitumia elimu wanayoipata kama nyenzo ya kupambana na maisha na kuachana na mwelekeo wa sasa ambapo wengi katika elimu ujikita kwa ajili ya kufaulu kwa viwango vya juu tu

Mkuu huyo wa mkoa Mongella ametoa wito huo katika mahafali maalumu ya Jumuiya wa wanafunzi vyuo na vyuo vikuu ambao ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) katika Mkoa wa Arusha

Mongella ametumia zaidi ya saa mbili kuwasisitizia kwamba kinachotakiwa kwa wahitimu wa vyuo na vyuo vikuu ni kujiwekea malengo kwa elimu wanayoipata kwa ajili ya maisha yao kwa kujitengenezea sifa za ziada badala ya kubeba shahada zao vichwani

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa(MNEC) ya CCM Anna Msuya ameeleza kuwa chama hicho kimeweka mipango mahsusi ya kuwaandaa vijana wasomi

Kwa upande wao Mwenyekiti wa Seneti ya jumuiya ya wanafunzi hao Baraka Solomon na Katibu wake Wema Somba wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuja na mpango wa kuanzishwa kwa Benki ya Vijana itakayokuwa suluhisho la vijana kujiajiri

Jumla ya wahitimu 350 ambao ni wanaCCM kutoka Vyuo na Vyuo Vikuu 17 katika mkoa wa Arusha wametunukiwa vyeti katika mahafali hayo

Share To:

Post A Comment: