Wednesday, 28 July 2021

MHANDISI MARYPRISCA AMUAGIZA KATIBU MKUU WIZARA YA MAJI KUTOA MIL.700 KUKAMILISHA MRADI WA MAJI MWANAMBAYA

 

 

NAIBU waziri wa maji ,Eng.MaryPrisca Mahundi amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo, atoe fedha za malipo kiasi cha sh .milioni 700 zilizoombwa na Wakala wa usambazaji maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Mkuranga ili kukamilisha ujenzi wa tanki la mradi wa maji Mwanambaya.

Ameeleza mradi huu ni miongoni mwa miradi itakayonufaisha watu wengi kwani unakwenda kutoa huduma na kunufaisha watu 8,000 .

MaryPrisca alitoa maagizo hayo wakati alipotembelea mradi wa chanzo cha maji Mwanambaya na tanki,na kueleza fedha hiyo imeombwa mwezi Juni hivyo wavute subira ,katibu mkuu afanyie kazi .

"Niisitize miradi inayoelekezwa kutoa huduma kwa wananchi tunaendelea kuitolea fedha kwa awamu hadi ikamilike ili kutimiza adhma ya serikali ya kumtua ndoo mama kichwani na kuondosha kero sugu ya ukosefu wa upatikanaji wa maji

Hata hivyo ,ameielekeza RUWASA Mikoa na Wilaya kukamilisha miradi viporo kwa wakati ili kurahisisha kazi ya usambazaji kwa wananchi .

Pia MaryPrisca ,aliwaelekeza mameneja wa RUWASA mikoa na wilaya kuhakikisha jumuiya za watumiaji maji vijijini wanapata watunza hazina makini waliosoma uhasibu na kupata cheti ama diploma ili kutunza miradi mbalimbali na iwe endelevu .

Nae meneja wa RUWASA wilaya ya Mkuranga Maria Malale alisema ujenzi wa mradi Mwanambaya umegharimu bilioni 2.3 ambapo bilioni 1.1 amelipwa mkandarasi 

Alisema mradi umefikia asilimia 90 ,mkandarasi anaendelea na kazi licha ya kupelea fedha milioni 700 ambayo wameshaiombea fedha kwa ajili ya malipo.

Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Hadija Ally alisema ipo miradi inayoendelea ambapo ikikamilika yote hali itakuwa safi na wananchi watanufaika kwa kiasi kikubwa na upatikanaji wa maji mjini ni asilimia 86 na vijijini ni 76.

Katika ziara hiyo ya kikazi ,MaryPrisca alitembelea na kukagua pia mradi wa maji Mkerezange ambao umekamilika na upo kwenye matazamio .
 

No comments:

Post a Comment