Afisa Masoko wa TBS, Rhoda Mayugu akimhudumia mmoja wa watu waliohudhuria kwenye banda lao katika maonyesho hayo ya Wiki ya Maziwa mjini Tanga
Afisa Udhibiti wa TBS, Emmanuel Bashakaya akimhudumia mmoja wa wadau wa maonyesho ya  wiki ya maziwa yaliyofanyika mjini Tanga

 
NA MWANDISHI WETU
 
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limewaasa wananchi kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake ili kuweza kuepukana na athari mbalimbali wanazoweze kukutana nazo kutokana na kununua zile ambazo hazijathibitishwa
 
Afisa Masoko wa TBS, Rhoda Mayugu alisema hayo katika maonyesho ya Wiki ya Maziwa yanayoendelea kwenye viwanja vya Tangamano Jijini Tanga. 
 
Rhoda anasema kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake.
"Tumetumia maonyesho haya kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida ya kutumia bidhaa zilizothibitishwa ubora wake," anasema Rhoda.
 
Akizungumzia maonyesho hayo yaliyoanza tangu Mei 31, mwaka huu na yanatarajiwa kufungwa leo, Rhoda amesema lengo kushiriki lilikuwa kuwafikia wadau wa maziwa na kuwapatia elimu kuhusu umuhimu na faida ya kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.
 
 Rhoda anasema wamefurahishwa na mwitikio wa wahudhuriaji wa maonyesho hayo na utayari wa kuthibitisha ubora wa bidhaa zao.
 
"Tumefurahishwa na mwitikio wa wengi waliohudhuria maonyesho hayo kuwa tayari kuthibitisha ubora wa bidhaa zao na hata wale ambao hawajathibitisha wako kwenye mchakato wa kufanya hivyo," anasema Rhoda.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: