Na Imma Msumba

Mwenge wa Uhuru maalumu umeanza kukimbizwa katika mkoa wa Arusha ambapo utakapokuwa mkoani hapa utaweka mawe ya msingi,kuzindua, kufungua na kukagua miradi 53 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 581.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongella amepokea Mwenge huo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere katika kijiji cha Kansay kilichopo wilaya ya Karatu.

Mwenge wa Uhuru maalum umeanzia wilaya ya Karatu kwa kupita katika miradi nane yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilion 3.4

Miongoni mwa miradi hiyo ni wa Ujenzi wa maabara katika kituo cha afya cha Endabash pamoja na mradi wa matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(Tehama) .

Kiongozi wa wakimbiza Mwenge kitaifa Luteni Josephine Mwambashi akapokea taarifa,akakagua na hatima kufungua au kuzindua mara baada ya kutoa maeleko ya namna bora ya kuboresha miradi hiyo

Mwenge huo utakuwepo katika mkoa wa Arusha kwa siku sita katika wilaya sita ukikimbizwa kwa jumla ya kilometa 950.35

Share To:

Post A Comment: