Na Mwandishi Wetu 


WADAU wa Maendeleo katika Jiji la Arusha  wameungana na Meya wa Jiji la Arusha , Madiwani pamoja na Wataalam wa Halmashauri  ya  Jiji la Arusha katika  uzinduzi wa Kampeni ya Usafi wa mazingira katika soko la Kilombero.


 Kampeni hiyo ni mwanzo na muendelezo wakufanya usafi katika Kata 25  za Halmashauri ya Jiji la Arusha 


Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqhe alisema kuwa lengo kampeni hiyo ni kuhamasisha usafi katika Jiji la Arusha na hatimaye kufanya Jiji la Arusha kuwa  mfano kwa mazingira safi ya Utalii na kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi .


Mhe. Maxmillian Iranqhe anasema ili kuandaa mazingira mazuri ya Utalii ni muhimu kila mmoja kujali usafi Kwa kufanya usafi katika Makazi wanayoishi na mahala pa kazi .


.Mh Iranqhe amewataka Wataalam wa Afya na Maafisa Afya kutoka ofisini nakwenda kusimamia usafi katika Kata za Halmashauri ya Jiji la Arusha


AmemtakaMkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa agizo hilo kwamba  usafi Jiji la Arusha unawezekana.


Mhe. Iranqhe ameongeza kwa kuwa usafi ni kichocheo cha maendeleo  na  fursa mbalimbali za kiuchumi kwa Wananchi pamoja na kivutio cha Utalii


 Katika  hatua Nyingine Mh .Meya alikabidhi vifaa vya usafi kwa Madiwani wa Kata 25 za Jiji la Arusha ikiwa nikuwezesha kuhamasisha wananchi wa Kata zao kufanya usafi katika Kata zao .


Denis Mwita ni Katibu wa Chama cha mapinduzi Wilaya ya Arusha anasema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa Viongozi na madiwani waliochaguliwa kupitia CCM wanania njema yakuleta maendeleo katika Jiji la Arusha .



Kampeni hiyo iliungwa mkono na wadau wa Taasisi mbalimbali wakiwemo NMB , TANAPA,CRDB , AICC, AZANIA BANK , ambapo baadhi ya Taasisi zilichangia vifaa vya usafi ikiwa ni matenki ya uchafu na mafagio ya Usafi

Share To:

msumbanews

Post A Comment: