MWENYEKITI  wa kamati ya  usalama barabarani  mkoa  wa  Iringa Salim  Asas amewataka  watumiaji  wa   vyombo  vya  moto  kuzingatia   sheria  za  usalama  barabarani  ili  kupunguza  ajali  za  barabarani.

Akitoa  wito   huo  leo  wakati  wa  uzinduzi  wa wiki  ya maadhimisho ya  Nenda  kwa  usalama barabarani  kwenye  viwanja  vya  stendi kuu ya  zamani ya  mkoa wa  Iringa ,Asas  alisema  kuwa  suala la  kufuata  sheria  za  usalama  barabarani  linapaswa  kuzingatiwa na  watumiaji  wote  wa  vyombo  vya  moto  ili  kuepusha  ajali  .

Alisema  imekuwa ni kawaida kwa madereva wa  piki piki maarufu kama  boda  boda  kujiona  wapo  juu ya  sheria  na  kuvunja sheria  za  usalama  barabarani  kusudi  jambo  ambalo  vyombo  husika  vya  usalama  havina budi  kuchukua  hatua .


Akizungumzia  suala la  madereva  kuomba  kusaidiwa  kupata mafunzo  mbali mbali  alisema  kuwa  suala  hilo linawezekana   hata kwa wao  wenyewe  kujikusanya na  kuomba  kupatiwa mafunzo hayo.

 

Share To:

msumbanews

Post A Comment: