MWENYEKITI wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa Iringa Salim Asas amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali za barabarani.
Akitoa wito huo leo wakati wa uzinduzi wa wiki ya maadhimisho ya Nenda kwa usalama barabarani kwenye viwanja vya stendi kuu ya zamani ya mkoa wa Iringa ,Asas alisema kuwa suala la kufuata sheria za usalama barabarani linapaswa kuzingatiwa na watumiaji wote wa vyombo vya moto ili kuepusha ajali .
Alisema imekuwa ni kawaida kwa madereva wa piki piki maarufu kama boda boda kujiona wapo juu ya sheria na kuvunja sheria za usalama barabarani kusudi jambo ambalo vyombo husika vya usalama havina budi kuchukua hatua .
Akizungumzia suala la madereva kuomba kusaidiwa kupata mafunzo mbali mbali alisema kuwa suala hilo linawezekana hata kwa wao wenyewe kujikusanya na kuomba kupatiwa mafunzo hayo.
Post A Comment: