Na,Jusline Marco:Arusha


Katibu Mkuu wizara ya Maji Mhandisi, Anthony Sanga amefungua mkutano wa wadau wa jukwaa la bonde la pangani Jijini Arusha wenye lengo la kujengeana uelewa na kutambua  mchango wa majukwaa ya bonde la Pangani katika usimamizi wa rasilimali za maji,ukiwa na kauli mbiu ya "Utunzaji wa vyanzo vya maji ni jukumu letu sote"


Akifungua mkutano huo Mhandisi Sanga amesema jukumu la wizara ya maji ni kuwapatia wananchi maji ya kunywa yaliyo safi na salama na kuhakikisha upatikanaji wa maji hayo unakuwa endelevu na kupatikana kwa wingi na kwa ubora unaokubalika.


"Jambo hili linategemea sana hatua stahiki zinazochukuliwa katika kuzitunza rasilimali hizo na kuhifadhi vyanzo vyake,hii ina maana kuwa iwapi hatutashirikiana na kutekeleza wajibu wetuipasavyo siku za usoni tutakuwa na miradi ya maji ambayo haitoi maji nchi itakuwa katika mtafaruku mkubwa. "Alisema Mhandisi Sanga


Aidha alisema kuwa bodi za maji na mabonde zimepewa jukumu la kusimamia vyanzo vya maji na kuhakikisha rasilimali za maji zinatumika kwa njoa endelevu na vyanzo vya maji kutunzwa ipasavyo kupitia sheria ya usimamizi wa rasilimali za maji namba 11 ya mwaka 2009.


"Sisi katika ngazi ya Wizara tunafuatilia kwa karibu kuhusiana na chanhamoto zinazoibuliwa na utekelezaji wake kwenye mabonde yote,niwahakikishie kuwa kama ambavyo tumeshafanya kwenye mabonde mengine tutadimamia kikamilifu mapendekezo mtakayoyatoa kuhusiana na changamoto zilizopo katika Bonde la Pangani."Aliongeza Mhandisi Sanga


Vilevile alieleza kuwa Bonde la Pangani ni bonde ya kwanza lililoanzishwa kwa majaribio wakati mfumo wa usimamizi wa rasilimali za maji likifuatiwa na bonde la Rufiki kupitia mabonde ya maji na kufanyiwa majaribio nchini na mfumo huo unatumika kwa Tanzania Bara pekee ambapo mfumo huo ulitokana na kuwepo kwa changamoto zinazohusiana na matumizi ya maji kwenye eneo hilo kanda ya Kaskazini ukilinganisha na maeneo mengine nchini.


Aliongeza kuwa pamoja na  bodi ya maji bonde la Pangani kuunda majukwaa mengine madogo madogo matano(5),majukwaa hayo yanafanya kazi karibu na Jumuiya ya watumia maji 22 zilizoundwa kwenye maeneo mbalimbali ambapo ameelekeza kuendelea kuimarisha ushirikishwaji wa wadau katika maeneo mengine ambapo majukwaa hayo hayajaundwa ili kuweza kuibua changamoto zinazotokea kwenye maeneo yao ambayo yatakuwa yakijadiliwa katika jukwaa la kimkakati.


"Uchumi na ustawi wa wakazi wa Bonde la Pangani unategemea kwa kiwango kikubwa usimamizi bora wa vyanzo vyetu vya maji hivyo kwa kuwa sote ni wanufaika wa vyanzo vya maji hatuna budi kushiriki kikamilifu katika kilinda rasilomali hii muhimu kwa kujiepusha na shughuli mbalimbali zinazoweza kuathiri wingi,ubora au uendelevu wake."Aliongeza Mhandisi Sanga


Pamoja na hayo Mhandisi Sanga ameeleza jitihada ambazo bonde linachukuwa katika kutunza na kuhufadhi vyanzo vya maji ikiwemo uwekaji wa alama za mipaka,mabango ya makatazo ya kufanya shughuli za kibinadamu katika hifadhi ya vyanzo vya maji,mabango ya kutambulisha mito maeneo ambayo barabara inakatisha  ambapo takribani mabango 150 yamewekwa,miti zaidi ya elfu 30imeoteshwa katika vyanzo vya maji na alama sa mipaka 1823,vilevile elimu juu ya usimamizi wa rasilimali za maji imetolewa katika naeneo mbalimbali.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara Rasilimali za maji katika Mkutano huo Injinia Mbogo Futakamba amesema suala la kushirikisha wadau katika usimamizi wa rasilimali za maji ni suala la kisheria,sera ya maji ya Taifa ya mwaka 2002 kutekeleza dhana ya usimamizi shirikishi qa rasilimali za maji,kifungu cha 3.2 ambapo majukwaa hayo ya sekta mtambuka yamekuwa rasmi kisheria kupitia maboresho ya kanuni za usimamizi wa rasilimali za maji na uteuzi wa wajumbe wa bodi.


Ameongeza kuwa majukwaa hayo yamewaleta wadau pamoja ili waweèèze kujadili changamoto mbalimbali za rasilimali za maji katika maeneo yao kwa kushirikishana na kubadilishana uzoefu ili usimamizi wake uwe endelevu hali itakayosaidia uboreshaji wa maji katika wingi na ubora unaokubalika kwa ajili ya matumizi ya kizazi cha sasa na cha baadae.


Naye Mkurugenzi wa Bonde la Pangani Segule Segule alisema rasilimali maji ili ziwe endelevu lazima zisimamiwe kuanzia kwenye vyanzo vya maji hadi habarini yanapoishia ambapo kufuatia hayp serikali iliona umuhimu kuanzisha majukwaa hayo kwa kushirikia na kutoa michango na mawazo katika kutunza rasilimali za maji ziweze kuwa endelevu.


Hata hivyo Segule ameeleza kuwa majukwaa hayo ambayo yameundwa katika ngazi ya kidakio ili kuweza kufikisha huduma za maji kwa wananchi ambapo lengo la mkutano huo ni kushirikishana changamoto na fursa mbalimbali kusudi kuweza kutoka na mkakati ambao utafanya rasilimali za maji kuwa endelevu.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: