Na,Jusline Marco;Arusha


Waziri wa fedha na mipango Dkt. Mwigulu Nchemba anatarajiwa kufungua mkutano wa 26 wa wanahisa wa benki ya CRDB utakaofanyika mei 22 mwaka huu Mkoani Arusha  katika ukumbi wa mikutano ya kimatafa(AICC).


Akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela kuhusiana na mkutano huo amesema kuwa mkutano huo utatoa fursa kwa wanahisa kujadili mwenendo wa benki hiyo na jinsi inavyofanya kazi zake.


Aidha kutokana na changamoto ya COVID 19 iliyoikumba dunia nzima Benki ya CRDB iliweza kubuni njia mbadala ya ufanyaji wa mikutano yao ambapo kwa kipindi cha mwaka jana waliwwza kufanya mkutano mkuu wa 25 kwa njia ya tehama.


Aidha Nsekela alisema kuwa baada ya kodi, benki hiyo iliweza kupata faida ya shilingi Bilioni 165 sambamba na kupungua kwa asilimia 4.4 ya mikopo chechefu ukilinganisha na miaka iliyopita ambapo mafanikio hayo yanayokana na ueledi wa usimamizi wa kitengo cha mikopo na ukaribu uliopo kati ya benki hiyo na wateja wao.


Aliongeza kuwa katika kipindi cha mwaka huu benki hiyo inatarajia kulipa shillingi 22 za gawio kwa wanahisa wake ambapo kwa mwaka jana waliweza kutoa gawio shilingi 8 kwa wanahisa hivyo ongezeko hilo linaenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu ya Pamoja,hatua kwa hatua.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: