Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (katikati), Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof Shukran Manya (kulia) na Mkurugenzi Mkurugenzi Idara ya Mtangamano wa Biashara ya wizara Bw. Ali Gugu (kushoto) wakishiriki Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma.

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo (kulia) akisikiliza kwa makini mjadala wakati wa Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao 23/04/2021, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mtumba, Dodoma.


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof Shukran Manya ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa 37 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri kwa Sekta za Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 23 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.

Mkutano huo wa 37 ulilenga kujadili uendelezaji wa Sekta ya Viwanda katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kuzingatia maelekezo yaliyopita ya Wakuu wa Nchi na Baraza la Mawaziri la Jumuiya kupitia mikutano mbalimbali iliyopita na kwa kuzingatia utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, Mkutano huo ulihudhuriwa na nchi zote sita (6) Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, na Sudani Kusini ulikuwa chini ya uenyekiti wa Jamhuri ya Kenya na Katibu wa Mkutano huo alitoka nchi ya Burundi.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Prof. Kitila Mkumbo (Mb.), aliyeambatana na Naibu Waziri wa Madini Mhe. Prof. Shukurani Manya (Mb.) ulijumuisha Maafisa Waandamizi kutoka Wizara za Viwanda na Biashara; Wizara ya Fedha na Mipango; Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Kilimo; Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) na Wizara Madini.

Pia, Mkutano huo wa 37 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji ulitanguliwa na mkutano ngazi ya Watendaji Wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika sekta hizo uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 22 Aprili, 2021 na ngazi ya Wataalam wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mahsusi katika eneo la Viwanda uliofanyika kwa njia ya mtandao kuanzia tarehe 20 hadi 21 Aprili, 2021 katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, uliopo katika Mji wa Magufuli Mtumba, Jijini Dodoma.

Ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya wataalamu katika mkutano huo uliongozwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na ulihudhuriwa na Wataalam kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Wizara ya Viwanda na Biashara, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Madini, Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Chama cha wazalishaji nguo na bidhaa za nguo Tanzania (TEGAMAT) na Mfamasia Mkuu wa Serikali.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: