Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo jioni ya leo tarehe 30 Aprili, 2021 ameripoti Ofisini na kuendesha kikao maalum cha utambulisho kwa Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa katika  Ofisi za Makao Makuu ya Chama Dodoma.


Pamoja na wajumbe wengine wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC), Kikao hiko kimehudhuriwa na Wajumbe wapya akiwemo Naibu Katibu Mkuu - Bara Ndg. Christina Mndeme na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka.


Kikao hiko maalum cha utambulisho, pia kimejumuisha viongozi wastaafu wakiongozwa na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM -  Bara Ndg. Rodrick Mpogolo na aliyekuwa Katibu wa NEC, Oganaizesheni  Ndg. Pereira Silima.


Imetolewa na, 

Said Said Nguya 

Afisa Habari Ofisi ya Katibu Mkuu

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

Share To:

msumbanews

Post A Comment: