Na Heri Shaban
MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto amekabidhi Photocophy mashine Shule ya Msingi Vingunguti Miembeni Wilaya Ilala leo.
Photocopy hiyo mashine imetolewa na wadau wa elimu Kampuni ya PMM ya Dar es salaam ambayo inaunga mkono juhudi za Meya Kumbilamoto katika kuisaidia serikali katika sekta ya elimu.
"Shule ya Msingi Vingunguti Miembeni imekuwa ikifanya vibaya katika mitihani katika shule hii leo nimekabidhi photocopy Mashine itumike kwa ajili ya shughuli za shule pamoja na kuburuza mitihani ya majaribio ya kuwapima wanafunzi ili kukuza kiwango cha sekta ya elimu watoto wetu wafanye vizuri katika masomo yako "alisema Meya Kumbilamoto
Kumbilamoto alisema awali amepata mdau wa elimu amewesha chakula kwa wanafunzi 9000 wa shule za wilaya hiyo ambapo mara baada shule hizo kuwezeshwa chakula wanafunzi wanafanya vizuri katika mitihani yao ya MOCO na Taifa.
Aliwataka wanafunzi kuzingatia masomo ili waweze kufanya vizuri wawe viongozi wa baadae.
Alisema Taifa lolote ili liweze kuendelea lazima watu wake wasome amewapongeza wadau wa Kampuni ya PMM katika kukuza kiwango cha elimu.
Aliwataka wazazi wawasimamie watoto wao wasome kwa bidii waweke na utaratibu wa kukagua madaftari yao wanapotoka shule waache tabia ya kubeti
Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Halmashauri ya Jiji Abrah Nchia alimpongeza Meya Kumbilamoto kwa juhudi zake kwa kujitoa katika sekta ya elimu amewataka wazazi kuacha urithi wa watoto wao wa Elimu.
Mkurugenzi wa Kampuni ya PMM Estates 2001 Ltd Mhina Mhina alisema anashirikiana na serikali ya Wilaya Ilala katika kuunga mkono juhudi za Serikali katika sekta ya elimu.
Mwisho
Post A Comment: