Na Woinde Shizza, ARUSHA.


MAHAKAMA , kuu masijala Ndogo ya kazi Kanda ya Arusha leo imeahirisha kesi ya madai dhidi ya kampuni ya Tan communication inayomiliki kituo cha  Radio Five baada ya upande wa wadaiwa kutokuhudhuria mahakamani na kushindwa kutoa taarifa.

Hakimu mkazi , Nguvava,ameahirisha kesi hiyo ambayo ilikuwa kwa ajili ya kusikiliza pingamizi lililowekwa na upande wa wadaiwa  hadi Juni 11 mwaka huu.

Wafanyakazi Saba wa radio hiyo wakiongozwa na Jofrey Steveni,walifungua kesi namb 151 ya mwaka 2020, wakikidai kituo hicho cha utangazaji cha radio five zaidi ya sh, milioni 31.9 baada ya kuachishwa kazi kinyume na utaratibu.

Wafanyakazi hao walifungua kesi mahakamani hapo baada kutoridhika na uamuzi uliotolewa na mahakama ya usuluhishi (CMA) baada ya kumpa ushindi mdaiwa.

Upande wa walalamikaji wanaongozwa na wakili Heri Makando waliiomba mahakama hiyo itoe idhini ya kukamatwa Mali za mdaiwa ambaye ni Tan Communication na kupigwa mnada ili kufidia malipo ya wafanyakazi hao.

Wafanyakazi hao waliomba mahakama hiyo itoe amri ya kukamatwa kwa Mali za mdaiwa,ambazo ni pamoja na Jengo la kituo hicho cha utangazaji cha Radio five,lililopo Njiro plot namb 153 n.a. 154 block J,Genereta ,vifaa vya studio pamoja na vifaa vya kufusyia  matangazo.

Upande wa mdaiwa,ambao uliwakilishwa na wakili ,Andrew Maganga aliwasilisha notisi mahakama kuu ya rufaa kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na jaji Johannes Masara , June 16 ,2020 iliyowapa ushindi wadai.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: