KATIBU Msaidizi wa Mkoa wa Kagera Mansoor akikabidhi msaada wa taulo za kike kwa ajili ya wafungwa wa Gereza la Bukoba Manispaa zilizotolewa na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira kwa  matumizi ya mwaka mzima
TIMU ya Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia NGOs Neema Lugangira na Uongozi wa UWT Mkoa na Uongozi wa UWT wilaya ya Bukoba Manispaa mjini kabla ya kutoa msaada kwa wanawake Gezerani Bukoba leo



BOX lilokuwa na Taulo za Kike za Kutosha za miezi sita za wanawake 53 waliopo Gezera la Bukoba

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh Neema Lugangira leo ametoa msaada wa taulo za kike kwa wanawake 53 ambao ni wafungwa waliopo kwenye Gereza la Bukoba lilipo Manispaa  ambazo watazitumia kwa kipindi cha miezi sita


Katika tukio hilo la Makabidhiano ya taulo hizo Mh Mbunge Neema ambaye yupo Dodoma kwa majukumu ya Kibunge, msaada huo ulikabidhiwa na leo na timu ya Ofisi ya Mbunge ikiongozwa na Katibu Wake Kitaifa Judith, Katibu Msaidizi Kagera Mansoor na Mratibu wa Ofisi Datius. Aidha, Chama Cha Mapinduzi kupitia Umoja Wanawake Tanzania kiliwakilishwa na Paulina ambae ni Katibu wa UWT Kagera, Sharifa ambae ni Katibu wa UWT Bukoba Mjini na PS wa Ofisi ya UWT Mkoa. 

 

Katika salamu zake Mh Mbunge Neema aliwatakia heri wanawake wote kote nchini kwa kuazimisha siku ya wanawake duniani huku akihaidi kwamba atakikisha mtoto wa kike hakosi shule kwa sababu ya kukosa taulo za kike na kwamba ushiriki wake katika ziara ya Kamati ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Madawa ya Kulevya ulimpa fursa ya kufika kwenye Gereza 2 (Njombe na Mbeya) hivyo kumfanya atambue uhitaji wa taulo za kike pia kwa wanawake walio gerezani na ndio maana akaamua kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa mtindo huu.  

 
Mbunge  Neema  aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo alisema suala la hedhi salama ni moja ya vipaumbele vyake hivyo ataendelea kutafta mbinu mbalimbali za kupunguza changamoto hiyo.


Aidha pia Mbunge Neema aliwasihi wanawake wajitambue na kujithamini ikiwemo kufanya kazi kufa na kupona yaani kwa bidii kubwa sana ili waweza kupata maendeleo

 

Akizungumzia mambo ambayo anakusudia kuyafanyia kazi Mbunge Neema alisema mambo ambayo atakwenda kuyafanyia kazi ni kupaza sauti na vipaumbele vyake vikubwa kwenye maeneo ambayo hayatiliwi mkazo kutokana na  kuona kwa sasa  ni wanawake wengi wanatesaka kwa kuachwa na mzigo mkubwa wa kulea watoto peke yao.

Alisema pili ni wanawake wengi wanafanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi lakini pia ni wafanyabiashara wadogo na wakienda kwenye mabenki kutafuta mikopo hawapati.

Alisema jambo hilo limekuwa likiwapa vikwazo vikubwa sana kwao kufikia maendeleo kutokana na kwamba wanapewa sheria kedekede ambazo hawaziwezi na moja ya kujukumu lake ni kutathmini wafanye nini ili wanawake walio kwenye sekta isiyorasmi waweze kuingia kwenye sekta iliyorasmi na waweze kupata mikopo ambayo itawasaidia kuwainua kiuchumi.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: