WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa akisisitiza jambo leo Bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali papo kwa hapo ya wabunge
Mbunge wa Viti Maalumu ( CCM) kupitia NGOs Mh Neema Lugangira akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa ikitumia Balozi zake za nje kutangaza mazao yaliypo ndani ya nchini ili kuweza kuyauza kwenye nchi ambazo wanatumia mazao hayo hatua ambayo imepelekea kupata wateja wengi kuja kununua hali iliyosaidia kuimarika kwa masoko.

Aliyasema hayo Bungeni Mjini Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa hapo la Mbunge wa Viti Maalumu ( CCM) kupitia NGOs Mh Neema Lugangira ambapo aliuliza kutokana na uwepo tatizo kubwa la masoko ya mazao yaliyopo nchini hata kama wakulima wanazalisha kwa ubora wa hali ya juu.

Je Serikali ipo tayari kupelekea wataalamu wake kwenye nchi ambazo zimefanikiwa ili kujifunza namna bora ya usimamizi wa masoko yaliyopo

Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba muhimu ni kutafuta mfumo mzuri unaowezesha mazao yaliyopo kujulikana na kuyauza kwenye nchi ambazo kuna wateja na wapate bei nzuri kama ilivyo ndani ya nchi uwepo mfumo wa stakabahdi ghalani ambao unakusanya mazao pamoja na kuwaalika wanunuzi wanakuja kila mmoja anatamka atanunua zao hilo kwa bei gani hivyo yule mwenye bei ya juu anapata fursa kununua.

Alisema kwamba huo ni ni mfumo uliondaliwa kwa ajili ya uuzaji wa mazao na utakuwa na bei nzuri huku akieleza pia Serikali ina mpango wa kutafuta masoko kwenye nchi ambazo zinazohitaji mazao hayo ili kuhakikisha wakulima wananufaika na kuweza kujikwamua kiuchumi

 “Juzi nilikuwa na Wabunge wa Mkoa wa Rukwa wakiomba Serikali iwasaidie kufika nchi ya Kongo, Zambia, Rwanda na Burundi kutafuta masoko ya mazao yanayolimwa mkoani humo” Alisema Waziri Mkuu

Aidha alisema kazi inayofanywa kwa sasa na Serikali ni kuhakisha inawasiliana na nchi ambazo ni walaji wa mazao hayo ili kujihakikisha mazao hayo yanapolimwa na kuvunwa yanapelekwa kwenye nchi zao na hiyo ni njia ya kupata soko nzuri la mazao pamoja na ubora unaofanywa.

Alisema kwa sasa Serikali itaendelea kujenga masoko ya kimkakati na ya kikanda ambayo yanalengwa pembezoni mwa nchi ili kukaribisha waliopo jirani kwenda kununua mazao yanayozalishwa hapa nchini

“Lakini miezi mitatu iliyopita nilikuwa Kilimanjaro pale Holili wanajenga soko kubwa sana ambalo wananchi wanaozalisha mazao yanapelekwa hapo na watu wa nchi jirani watakwenda hapo kununua  na wanawapunguzia ugumu wa kuingia mpaka ndani”Alisema

Hata hivyo alisema mwezi mmoja uliopita alikuwa mkoani Kigoma ambapo eneo Kagunda wamejenga soko nzuri wanawakaribisha majirani watu wa Burundi na Rwanda kwenye kununua jambo ambalo linapunguza umbali wa kufuata bidhaa.

Sambamba na hilo alieleza kwamba hivi sasa Serikali inajenga soko kubwa mkoani Kagera eneo la Nyakanazi lengo wale wanaotoa Kongo, Rwanda watafika kwenye soko hilo la zaidi ya Bilioni 3.5 ili waweze kupata bidhaa na muhimu ni kuweka mkakati wa namna mazao yaliyoboreshwa na kupata thamani kubwa ili yaweza kupata thamani kubwa ili kumuwezesha mkulima aweze kupata tija kwa kazi ya kilimo anayoifanya.

Mwisho

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: