Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Dkt. Consolata Ishebabi akizungumza wakati akifungua mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara hiyo mafunzo yanayolenga kuongeza ubora kazini, yaliyofanyika leo Februari 23,2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini, Dodoma.
Mkufunzi wa KAIZEN ambaye pia ni Meneja wa SIDO wa Mkoa wa Dodoma Bw. Sempeho Manongi akitoa mada kuhusu Utekelezaji wa KAIZEN kwa watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara mafunzo yaliyofanyika leo Februari 23,2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini, Dodoma.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya KAIZEN kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara wakifuatilia maada zilizokuwa zikiwasilishwa na wakufunzi wakati wa mafunzo ya KAIZEN yaliyofanyika leo Februari 23,2021 katika ukumbi wa Chuo cha Biashara (CBE) jijini, Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Viwanda Vidogo Dkt. Consolata Ishebabi wa pili kutoka kulia waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo hayo mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika leo Februari 23,2021 katika ukumbi wa Chuo cha biashara (CBE) jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Dkt. Consolata Ishebabi amewaasa watumishi wa Wizara ya Viwanda kutumia mafunzo ya KAIZEN katika kuongeza tija na ubora katika utendaji kazi na katika majukumu yao ya kila siku.
 
Kaimu huyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Viwanda Vidogo wa Wizara ya Viwanda na Biashara ameyasema hayo Jijini Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo ya KAIZEN kwa watumishi wa Wizara hiyo yaliyofanyika leo katika Chuo cha Biashara CBE jijini Dodoma, amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwawezesha watumishi wa wizara kubadili mtazamo, kuongeza tija uwajibikaji na ubora mahala pa kazi.
 
" Tuiweke KAIZEN katika mipango yetu kuanzia ofisini hadi katika familia zetu ili kuongeza tija na ubora katika utendaji kazi na maisha yetu ya kila siku na tujipime kwa kutumia vipimo vya utumishi kama OPRAS" . amesema Dkt Ishebabi.
 
Aidha, Mkurugenzi huyo amewasisitiza watumishi hao kutumia S tano ( 5) ambazo ni Sasambua (Sort), Seti (Seti), Safisha (Shine), Sanifisha (Standardize) na Shikilia (Sustain) katika kutekeleza 
 
KAIZEN mahala pa kazi na kwenye maisha yao ya kila siku.
Amesema mafunzo hayo pia yanalenga kuongeza ufahamu kuhusu mfumo wa falsafa ya uongezaji thamani endelevu wa tija na ubora viwandani ili waweze kushiriki kikamilifu katika kufanikisha utekelezaji wa falsafa hiyo katika sekta wanazozihudumia.
 
Dkt. Ishebabi pia amesema mafunzo hayo yanaongozwa na kauli mbiu isemayo "KAIZEN kwa Tanzania ya Viwanda Shindani kwa Maendeleo Shirikishi".
 
kauli mbiu hiyo inaendana na azma ya Serikali ya awamu ya tano inayodhamiria nchi yetu kuwa na uchumi wa kati wa Viwanda ifikapo mwaka 2025.
Mradi wa KAIZEN inayofadhiliwa JICA unalenga kuongeza tija na ubora katika sekta ya viwanda na shughuli za maisha ya kila siku inaongozwa na misingi ambayo ipo katika ubunifu wa mawazo, maarifa na ushiriki wa kila mtu ndani ya taasisi, shirika au kampuni.
KAIZEN ni neno la kijapani lenye maana ya badilika kwa ubora / uzuri linalohusu shughuli endelevu zinazofanyika ili kuboresha kazi mifumo michakato na nyanja yoyote ya kuendesha biashara. KAIZEN asili yake ni Japani lakini sasa inatekelezwa Duniani kote.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: