NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA


Halmashauri ya Arusha DC   imejipanga kuhakikisha kuwa wafanyabiamshara wakubwa hawachukui vitambulisho vya machinga bali wanalipa kodi inayostahili kwa  kuwapa elimu juu umuhimu wa kulipa kodi.



Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Ojung'u Salekwa wakati wakiongea na waandishi wa habari  leo ofisini kwakwe kuhusiana na mikakati ya namna gani watakukusanya mapato ya halmashauri na kuweza kufikia malengo waliojiwekea.


Alisema kuwa kumekuwepo na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kudanganya na kuchukuwa vitambulisho vya machinga ili kukwepa kukadiriwa kodi inayostaili,hali iliodababisha halmashauri hiyo kutofikia lengo la ukusanyaji wa mapato kwa Kota ya kwanza ya bajeti ya mwaka 2020/2021.


Ojung'u alieleza kuwa halmashauri imejipanga kutumia watalam wa ndani kutembelea biashara na kubaini maeneo ya wafanyabiashara wakubwa ili  kuweza kuwakadiria mapato yanayo staili na kuwathibiti wasiweze kuchukuwa vitambulisho vya machinga litakapoanza zoezi za ugawaji wa vitambulisho hivyo.



 "Tunashirikiana na  mkurugenzi pamoja na wataalam wetu kuwaelewesha na kuwaelimisha umuhimu wa kulipa kodi kwani wanapolipa kodi ni kwafaida yao ,kwani kodi hizo ndizo zinazotumika kuleta Maendeleo ya nchi ikiwemo kujengea barabara na vituo vya afya pamoja na huduma zingine za kijamii" alibainisha Ojung'u


Aliongeza kuwa wanasubiri vitambulisho vipya vya machinga vilivyoboreshwa na kuhakikisha kuwa watakao pewa ni wamachinga halisi na sio wafanyabiashara wanaokwepa kodi na kusababisha halmashauri kushindwa kufikia malengo yake



Aidha alifafanua kuwa mapato ndio roho ya halmashauri ambapo kuna maeneo ikiwemo eneo la uchimbaji wa mchanga la Osunyai,wamewaondoa baadhi ya mawakala na kuwaweka wanajeshi wa JKT Suma jambo ambalo limeshaonyesha matokeo chanya.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: