Tuesday, 2 February 2021

Lori Lagonga Treni Vingunguti, Dar es Salaam

 


Shirika la Reli Tanzania (TRC) limethibitisha kutokea kwa ajali ya treni leo alfajiri eneo la Vingunguti, Dar es Salaam ambapo gari la mizigo limeigonga treni kwenye kivuko cha reli na barabara.

TRC imeeleza kuwa katika ajali hiyo hakuna taarifa za kifo na kuwa majeruhi ni watatu, wote wafanyakazi wa TRC, na tayari wamepelekwa hospitali ya Reli Tanzania kwa matibabu.

Treni hiyo ya abiria (Deluxe) ilikuwa ikitokea mikoa ya Kigoma, Tabora, Dodoma na Morogoro na wakati wa ajali ilikuwa na abiria wapatao 828.

Shirika hilo mbali na kutoa pole kwa waliofikwa na ajali hiyo, limeendelea kusisitiza umma kuzingatia sheria za barabarani kwani dereva wa gari lililogonga treni alitakiwa kupunguza mwendo na kusimama umbali wa mita 100 alipokaribia kivuko hicho.

No comments:

Post a Comment