Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mashiba akitoa mada kwenye semina ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyoandaliwa na Mfuko huo wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Faustine Ndugulile akizungumza mbele ya wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso,akitoa neno la pongezi mara baada ya kumaliza kupewa mafunzo na elimu katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

Baadhi ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu wakitafilia semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ambaye ni Mbunge wa Ilala,Mhe. Musa Azan ‘Zungu’ akichangia katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora, Humphrey Polepole akichangia katika semina iliyoandaliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wenye lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo kuhusu mfuko huo iliyofanyika bungeni jijini Dodoma.

..................................................................................

Na Alex Sonna, Dodoma

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imesema itahakikisha inashirikiana na serikali ili Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) uwe na bajeti nzuri itakayosaidia kufikisha huduma za mawasiliano maeneo mbalimbali nchini hususan yaliyopo pembezoni na mipakani.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Selemani Kakoso ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza viongozi wa Wizara, Menejimenti ya Wizara na watendaji wa UCSAF katika semina kwa wajumbe wa kamati hiyo na baadhi ya wenyeviti wa kamati za bunge kuhusu huduma ya mawasiliano.

Akizungumza katika kikao hicho, Kakoso ameupongeza mfuko huo kwa utendaji mzuri wa baada ya Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Faustine Ndugulile kuwasilisha taarifa ya majukumu ya Mfuko huo.

Amesema wabunge wataendelea kuishauri serikali kuimarisha utendaji kazi wa mfuko huo ili kufikisha mawasiliano kwa wananchi.

Kwa upande wake, Dk.Ndugulile alisema kikao hicho ni kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo ili wafahamu majukumu ya UCSAF na kushirikiana na Wizara kuhakikisha kuwa UCSAF inatekeleza majukumu yake na kufikia malengo iliyojiwekea.

“Wizara hii inasimamia njia moja kuu za uchumi kama ilivyo Wizara ya Ujenzi inavyobeba barabara na Nishati inabeba umeme, na hii ni moja ya njia kuu za uchumi katika dunia ambayo tunakwenda nayo ili tuhakikishe kuwa tunajenga uchumi wa kidijitali kwa kuwa sasa hivi dunia imehamia kiganjani na Wizara hii itaratibu masuala yote ya TEHAMA ndani ya Serikali ili mwananchi apate huduma kwa wakati na TEHAMA ichangie kikamilifu pato la taifa,”amesema.

Naye, Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Kundo Mathew, amefafanua kuwa Wizara kwa kushirikiana na UCSAF na kampuni za simu za mkononi wataendelea kuboresha huduma za mawasiliano kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa kuongeza uwezo wa minara ya mawasiliano.

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Humphrey Polepole ameipongeza UCSAF kwa kujenga vituo vya TEHAMA kwenye kisiwa cha Unguja na Pemba ambapo vituo hivyo vinawawezesha wananchi kupata huduma ya intaneti karibu na maeneo yao na ameshauri ujenzi wa vituo hivyo uendelee kufanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Awali, Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Justina Mshiba amesema kuwa UCSAF itapita kwenye maeneo yote ya mipakani mwa Tanzania na kufanya tathmini ili kupata idadi ya minara inayohitajika kwenye maeneo hayo ili kuhakikisha kuwa maeneo ya mipakani yana mawasiliano ya uhakika.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: