Monday, 15 February 2021

Dr. Dugange azindua ugawaji wa vifaa vya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa KizaziNteghenjwa Hosseah, Mbeya


Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe.Dr Festo Dugange amezindua ugawaji wa vifaa vya uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi jijini Mbeya tarehe 13/02/2021.


Dr. Dugange amezindua ugawaji wa vifaa  vyenye thamani ya shilingi Mil 824 ambavyo vimetolewa na Shirika lisilo la Kiserikali la WRP-T.


Akizindua zoezi la ugawaji wa vifaa hivyo Dr. Dugange ameshukuru Shirika la WRP-T kwa kuwezeshabupatikanaji wa huduma bora ya VVU na Saratani ya Mlango wa kizazi kwa wananchi wa nyanda za juu kusini.


“Hakika WRP-T mmefanya kazi kubwa sana ya kutoa matunzo ya matibabu kwa watu wanaoishi na VVU na kutekeleza afua mbalimbali za kuweza kuimarisha Afya za Watanzania wenzetu.


Mmewezesha huduma ya Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi kusogezwa karibu zaidi na wananchi kama tunavyojionea hapa huduma hii inapatikana kwenye Kituo hiki cha Afya Kiwanja mpaka hii ni hatua kubwa sana katika utoaji wa huduma za Afya” alisema Dr. Dugange.


Wakati huo huo Dr. Dugange aliwataka watendaji wa Afya  kutumia vifaa hivyo kwa uangalifu na kuvitunza ili viweze kudumu muda mrefu na kuhudumia wananchi wengi zaidi.


Naye Mkurugenzi wa Afya Ustawi wa Jamii na Lishe Dr Ntuli Kapologwe amesema Serikali imefanya kazi kubwa katika kuboresha miundombinu ya huduma za Afya kuanzia kwenye ujenzi wa  Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya na Zahanati.


Kwa kutambua mchango wa wadau Serikali imegatua madaraka katika baadhi ya huduma za Afya mbapo

Wadau kama WRP-T wanashiriki katika kutoa huduma ya Saratani ya mlango wa kizazi na VVU alisema Dr. Ntuli.


“ Tumeona huduma hii ikitolewa kwa ufanisi Mkubwa katika Mikoa ile ambayo Mradi huu unafika wakinamama wanapata uchunguzi wa kina na wale wanaogundulika na ugonjwa huo hupatiwa matibanbubbure kabisa hii ni faraja kubwa kwetu kuona huduma hii inapatikana katika vituo vya kutolea Afyamsingi” alisema Dr Ntuli.


Naye Mkurugenzi Mtendaji wa WRP-T  David Dr. Maganga amesema wanaunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha Afya za Watanzania; Katika mapambano dhidhi ya Ukimwi lengo la 95-95-95 wamefikia 

asilimia 96 kwa watu waliopimwa VVU

asilimia 93 kwa waliogundulika na wameanza  tiba na asilimia 98 walioanza tiba na kufubaza virusi vya UKIMWI.


Aliongeza  kuwa WRP-T wamefanikiwa kusambaza mashine za kupima wingi wa Virusi vya UKIMWI (Viral load) 12 katika Mikoa minne ya mradi na wanaendelea na jitihada za kupunguza maambukizi mapya.


“Kwenye upande wa  Saratani ya mlango wa kizazi kwa mwaka 2019-20 wakinamama elf 38 wamepata huduma za kiuchunguzi na kwa mwaka 2021 tumepanga  kuwafikia wakina mama elfu 41. 


Leo hii vifaa vinavyogawiwa vina thamani ya shilingi Mil 800 na  vitawezesha kuboresha Tiba, Kinga na utambuzi wa Safatani ya Mlango wa kizazi katika maeneo mbalimbali. 


Halkadhalika tumehakikisha kuwa huduma ya kupima Vvu kwa Wanawake imeunganishwa na Uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi ili kuweza kutoa huduma kwa urahisi na Tiba mgando inapatikana kupitia vituo hivyo.


Mradi wa WRP-T unatekelezwa katika Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa, Katavi na katika Mkoa wa Ruvuma kwa huduma ya tohara tu.


Mwisho

No comments:

Post a Comment