Wednesday, 3 February 2021

CCM KIBAHA MJI YAJIPANGA KUONGEZA WANACHAMA WAPYA-LUAMBANO

 


Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Kibaha Mjini, mkoani Pwani, kimejiwekea
mkakati wa kuongeza wanachama zaidi kwa mwaka 2021-2022 ,ikiwa ni
pamoja na kumtaka kila balozi kuongeza wanachama wapya 25.

Aidha ,kimehimiza umoja na mshikamano kwa wanachama wake ili
kukiimarisha chama hicho .

Akizungumzia sherehe za kuadhimisha miaka 44 ya CCM tangu kuanzishwa
kwake ,Katibu wa CCM Kibaha Mjini, Afidu Luambano alisema mji huo una
jumla ya mabalozi 611 hivyo kwa kila mmoja kupata wanachama
wasiopungua 25 watakuwa wamepiga hatua kubwa.

Alibainisha, mabalozi ndio nguvu ya chama ,hivyo wataendelea
kushirikiana nao kwa kuhakikisha mikakati ya chama inafanikiwa na
chama kinasonga mbele.

"Chama chochote mtaji wake ni kuongeza wanachama wapya ambapo mwaka
2018 walikuwa na wanachama 39,000 na hadi kufikia 2019 Katika uchaguzi
wa serikali za mtaa,vijiji na vitongoji waliongezeka na kufikia
53,230." alifafanua Luambano.

Luambano aliwaasa wanachama na viongozi wa kata pia kuwa na ushawishi
kuongeza wanachama na kusisitiza umuhimu wa kulipa ada .

Pamoja na hayo alikemea makundi yasiyo na tija na kuomba umoja na
mshikamo uzidishwe baina yao .

Akielezea ,sherehe za kuadhimisha miaka 44 ya CCM ,Katibu huyo
alisema, wanahimiza kila kata kuchangia madawati mawili kwa ajili ya
kuchangia kupunguza tatizo la upungufu wa madawati kwenye shule za
sekondari ama shule za msingi Mjini hapo .

Hata hivyo ,kata itakayofanikiwa kwa maandalizi mazuri ya sherehe za
maadhimisho ya miaka 44 ya chama kitatoa zawadi ikiwa ni kama motisha

No comments:

Post a Comment