Mkuu wa Wilaya Ya Arusha Mh Kenani Kihongosi ameongoza jogging leo akiwa na wananchi wa Jiji la Arusha, amesisitiza Umoja Amani na Utulivu pia wananchi kujitolea kushiriki katika shughuli za Kizalendo.


Pia Mhe Kenani Kihongosi ameishukuru kampuni ya ASAS DIARIES MILK kwa sapoti kubwa yamaendeleo inayotoa kwa wananchi ikiwemo Ajira na huduma za Kijamii, amesema watazidi kuwaunga mkono kwani wanafanya kazi nzuri kwa jamii.

Amewashukuru wananchi wa Jiji la Arusha kwa namna ya kipekee na Amewaeleza atazidi kuwatumikia kwa nguvu zote bila kuchoka.

Mwisho Amempongeza na Kumshukuru Mh Rais Dr. JOHN POMBE MAGUFULI kwa Kuwaletea maendeleo makubwa wananchi wa Jiji La Arusha na amesema wananchi wazidi kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuchapa kazi kwa bidii kwani Mheshimiwa Rais Ameonyesha Nia ya dhati ya Kuibadilisha Tanzania kiuchumi hivyo lazima tumuunge Mkono.

Mtumishi wa Wote









Share To:

Post A Comment: