Tuesday, 1 December 2020

ULEGA AKAGUA UJENZI WA SHULE NA ZAHANATI VIKINDU


 Muonekano wa madarasa yaliyojengwa ya shule ya msingi katika Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga shule hii ujezi wake umegharimu shilingi milioni 400.
Mbunge wa Jimbo la Mkuranga,Abdallah Ulega akizungumza na viongozi mabilimbali wa wilaya ya Mkuranga wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali leo 


Muonekano wa sasa wa kituo cha Afya cha kata ya Vikindu Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga matumaini ya upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ujenzi wa kutuo hicho umegharimu shilingi Milioni 200.

 MBUNGE wa Jimbo la Mkuranga, Abdallah Ulega amefika katika Shule ya msingi Chatembo katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali.


Namshuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwatupa fedha za miradi ya kituo cha afya, Zahanati pamoja na Shule ya msingi Mwenyezi Mungu amlipe kilalililijema.

“Nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa kituo cha Afya cha kata ya Vikindu pamoja ujezi wa Zahanati ya kijiji cha Mwandege na shule ya msingi chatembo ikiyopo kwenye kata ya Mwandege.

Niwapongeze sana wananchi na wadau mbalimbali kwa ushirikiano wenu kushiriki ujenzi wa miradi hii ujezi wa kituo cha Afya Vikindu umegharimu Shilingi Millioni 200 ujenzi wa shule ya msingi umegharimu" Alisema Ulega

Shilingi Million 400 pesa zote zimetolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

No comments:

Post a Comment