Wednesday, 2 December 2020

TAHA KUFUNGUA FURSA YA MASOKO KILIMO CHA HORTICULTURE
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA. 


Asasi ya kilele inayojishughulisha na kilimo hoticulture yaani mboga mboga, matunda, mimes itokanayo na mizizi, pamoja na viungo (TAHA) imeandaa kongamano maalum la kufunga fursa za mazao hayo katika masoko ya ukanda na kimataifa.


Akiongea na waandishi wa habari hivi karibuni Mkurugenzi mtendaji wa Asasi hiyo Dkt Jackline Mkindi alisema kuwa  kongamano hilo linalotarajiwa kufanyika December 5 mwaka huu ni mahususi kwa watanzania wazalishaji ,wafanyabiashara,wasafirishaji,wasindikaji na wadau wa kilimo cha mbogamboga matunda,mimea itokanayo na mizizi pamoja na viungo kwani una lengo la kuhamasisha uwekezaji wa masoko katika mazao hayo.Dkt Mkindi alieleza kuwa kongamano hilo litakuwa na washiririki wakubwa zaidi ya 350 waliothibisha ushiriki wao kutoka nchi ya Tanzania,Comoro,Rwanda, Sudani, Kenya,DRC Congo pamoja na Malawi ambao kwa pamoja watajadili maendeleo ya sekta na mazingira endelevu ya biashara baina ya nchi zilizomo ukanda wa Afrika Mashariki na nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika na kuhamasisha fursa za uwekezaji na masoko katika mazao hayo."Washiriki watapata fursa ya tukutana na wadau wakubwa wa kilimo cha horticulture wa jumuiya ya Africa Mashariki(EAC) jumuiya ya madola ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC) kwa nia ya kuvutia uwekezaji na pia kutengeneza ushirikiano linganifu kati ya sekta hiyo hapa nchini na zingine za kanda za kibiashara za Afrika Mashariki na kusini,"Alisema Dkt Mkindi."Katika mkutano huo tutagusia baadhi ya maeneo na kuyajadili yatakayojadiliwa ambayo ni fursa za uwekezaji,masoko,sekta ya usafirishaji,mfumo baridi na viwezeshi vingine vitakavyosaidia upatikanaji wa masoko kama sehemu yakuendeleza nakukuza kilimo cha horticulture baina ya nchi hizi," Alifafanua.


Aliendelea kusema kuwa ikumbukwe kwamba hivi karibuni Rais wetu,Mh.John Magufuli alitaja sekta hiyo kuwa ni miongoni mwa sekta ndogo zinazokua kwa kasi zaidi hapa nchini kwani nchi yetu inashika nafasi 20 kwa kuzalisha kwa wingi mazao hayo duniani  na mauzo ya nje yameongezeka kutoka Dola za Marekani millioni 412 ya mwaka 2015 na kufikia Dola za Marekani million 779 mwaka 2018/2019.


Dr.Mkindi alisema masoko ya horticulture yanakua kwa kasi kwa upande wa zao la parachichi pekee thamani yake litapanda hadi kufikia dola za kimarekani milioni 23 hadi 26 kwani mazao hayo yanahitajika kwenye nchi za ulaya,ukanda wa Mashariki ya kati hata Afrika kutokana na baadhi ya nchi kutozalisha kilimo hicho.


"Nchi ya Tanzania ukiiangalia tuna uwezo wa kuzalisha kila aina ya kilimo cha horticulture ukianzia Matunda ya aina zote,mboga za kila aina,pamoja na viungo mbalimbali kuanzia vitunguu swaumu na tangawizi kwani tumekuwa na oda nyingi za uhitaji wa matunda baada ya ugojwa wa korona,"Alisema."Natoa wito kwa wadau wa sekta hii kuendelea kujisajili kupitia www.taha.or.tz kwa kujifunza ,kuboresha shughuli za tasnia hii yahorticulture keisha kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi nchini,"Alisema.


Hata hivyo kongamano hilo litafanyika katika ukumbi wa hotel ya Hyatt Regency Mary kama The Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment