Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi akiangalia Samaki wanafugwa na kutunzwa katika kituo cha Shanzan Njiro ,Halmashauri ya Jiji la Arusha na mwekezaji wa shamba hilo Zainali Bhima akielezea jinsi wanavyofuga samaki kwa njia ya kisasa


Na Mwandishi wetu


SERIKALI imesema kuwa itawezesha vijana kuanzisha miradi ya ufugaji wa samaki wa njia ya kisasa ikiwa ni hatua mojawapo ya kuwawezesha kujiajiri na kuondokana na tatizo la ajira kwa vijana na kwamba wadau wa ufugaji wenye nia yakufundisha vijana kupata ujuzi wa ufugaji wa kisasa watapewa ushirikiano wa karibu ili waweze kufanikisha nia njema ya kuwapatia vijana ujuzi kwa kushirikiana na serikali .


Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi Mh  Pauline Philipo Gekul akizungumza katika  kituo na shamba  la uzalishaji Samaki wa njia ya kisasa kinachojulikana  kwa jina  la Shanzan kilichopo Njiro ,Halmashauri ya Jiji la Arusha alisema kuwa mikopo wa Vijana inayotolewa katika Halmashauri wa asilimia 4 inatakiwa kutumiwa  kuanzisha  mradi kama huo wa ya ufugaji wa samaki wa kisasa  .


Mh  Gekul alitaka vijana kujitokeza kuchangamkia fursa ya ufugaji  kwamba Serikali inania ya kuongeza ajira kwa vijana kuwa ufugaji ni njia mojawapo ya kuajiri Vijana .


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dk.John Pima alisema kuwa tayari Halmashauri ya Jiji la Arusha imeanza mkakati wa ufugaji wa kisasa na kwamba mikopo ya makundi maalum ya vijana ,wanawake na walemavu itaanzisha miradi mikubwa kama ufugaji wa kisasa wa Samaki na kuhimiza makundi hayo kujitokeza ili kupatiwa elimu na fedha za kuanzisha miradi hiyo .


Dk.Pima anasema kuwa kuwa tayari Tshs zaidi  million 500 zipo kwa ajili ya kukopesha makundi maalum ya Halmashauri hiyo na kuhimiza Vijana kujitokeza wakiwa wamejiunga kwenye vikundi na kuandaa mpango bora wa mradi husika ili kuweza kupata mkopo wa kuanzisha ufugaji bora utakaowaondolea umaskini.


“Sasa hivi hatutoa fedha ,tutatoa fedha kwa ajili ya miradi  na vifaa ,niwaombe makundi maalum kuja na mpango bora kuibua mradi wanaodhani utawawezesha kufikia malengo ya mafanikio “alisema Dk.Pima


 Naye ,Naibu Meya wa Jiji la Arusha Mh. Veronika Hosea akizungumzia mradi huo alisema kuwa kwa kushirikiana na madiwani wenzake ,watahakikisha wanahamasisha ufugaji  wa samaki kwa njia ya kisasa kwa kuwa unaweza kufuga hata nyumbani na siyo lazima katika mabwawa ya samaki .


Mh. Hosea anasema kuwa Jiji la Arusha linajivunia kuwa na mfugaji wa samaki wa njia ya kisasa  kama huyo  kwamba atafundisha vijana na watu wenye nia ya kufuga kwa kisasa .


Zainali  Bhimani ,ambaye ni mwekezaji wa  wa Shamba la Samaki Shanzan Njiro ,anamuomba Naibu Waziri kumpelekea ombi la kusafirisha samaki kwenda maeneo mbali mbali nchini kwa bei nafuu kwa kuwa gharama za usafirishaji ni kubwa hali inayomfanya kushindwa kufikia malengo yake kwa haraka .


Bhimani aliongeza usafiri wa gari unachelewesha kufikisha mzigo haraka hali inayochangia samaki kuharibika kwamba usafiri utamuwezesha kufikia walengwa wengi hatimaye kuwezesha kuchangia uchumi wa nchi .


Pamoja na mambo mengine alisema kuwa yuko tayari kufundisha makundi mbali mbali namna ya ufugaji bora wa samaki kwa njia ya kisasa ambayo haitegemei mabwawa .

Share To:

msumbanews

Post A Comment: