Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini ambaye pia ni Naibu Spika Dr. Tulia Ackson amefanya ziara katika kata ya Sinde kwa lengo la kutembelea na kukagua mfereji wa maji wa Ilolo unaounganisha maji katika kata mbalimbali Jijini humo ambao umekuwa ukifurika na kusababisha madhara kwa wananchi ikiwemo kuharibu makazi.


Dr. Tulia amesema>>>”Leo nimekuja hapa kata ya Sinde kuangalia huu mrereji wa maji na nimepitia kwa sehemu ndefu ni kweli changamoto ni kubwa licha kwamba leo mvua haijanyesha lakini maji ni mengi maana yake yakiongezeka ya mvua changamoto itakuwa ni kubwa zaidi”


“Hili jambo nilishapata kulisikia huko nyuma na nikajaribu kulifuatilia na taarifa zilizopo ni kwamba mradi mkubwa wa kuondoa hili tatizo hapa utaanza kutekelezeka mwishoni mwa mwaka 2021, lakini ni lazima kwa mazingira haya tuchukue hatua kadhaa ili kupunguza hili tatizo”-Dr. Tulia Ackson


“Niwaombe wananchi kuwa watulivu wakati tukitafuta suruhu ya kudumu lakini lazima tuanze kukubaliana, siku ya Ijumaa tutakutana wote hapa kusafisha mfereji katika sehemu zilizotuama uchafu ili kusaidia maji kupita kwa wepesi na zoezi hili lazima litakuwa endelevu”-Dr. Tulia Ackson

Share To:

msumbanews

Post A Comment: