NA HERI SHAABAN


MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus amewataka wananchi wa Jimbo la Segerea kushirikiana na Watendaji katika kutatua kero za Wananchi  .


Mbunge Bonah aliyasema hayo Dar salaam jana wakati wa kuwashukuru Wajumbe wa Mkutano wa Jimbo la Segerea. 


"Nawaomba viongozi wangu wa Chama tushirikiane na Watendaji katika kutatua kero za wananchi kuanzia ngazi ya Mtaa hadi Kata ili kuondoa changamoto za wananchi wetu "alisema Bonah. 


Bonah alisema katika Jimbo la Segerea kuna changamoto mbalimbali ikiwemo Miundombinu ya Jimbo la Segerea hilo sio mizuri .



"Katika Jimbo hili  Kata 11 Miundombinu sio mizuri kata mbili Kiwalani na Minazi Mirefu ndio ina Barabara nzuri na miundombinu yake mizuri zikiwemo huduma za jamii za uhakika"alisema . 



Aliwataka  wananchi wa Segerea  kushirikiana katika kutatua kero za Wananchi kwa ajili ya kuleta maendeleo Segerea.



Aidha Bonah aliwataka Wananchi wa Segerea kuunga mkono juhudi za kazi zinazotekelezwa  na Mh, Rais John Magufuli katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi katika kujenga Tanzania ya uchumi wa viwanda.


Kwa upande wake mgeni rasmi, Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu aliwataka Viongozi wa Kata na Matawi kutatua kero za wananchi wa Jimbo la segerea. 


Alisema kero zinazoibuliwa ngazi ya Mtaa zitatuliwe kwa wakati kwa ajili ya kuisaidia serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM. 



Naye Meya wa Halmashauri ya Ilala alisema uchaguzi umekwisha sasa kikubwa kila mtu kufanya kazi na kusimamia maendeleo .



Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ni sikivu  amewataka Watendaji kila mmoja awe na Ilani ya Chama 2025 inayoelezea miradi ya kutekeleza ndani ya miaka mitano. 


Mwisho

Share To:

msumbanews

Post A Comment: