Na Marco Maduhu, Shinyanga
Shirika
la Voluntary Services Overseas (VSO), limetoa vifaa kwa wahitimu wa
fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stadi VETA mkoani Shinyanga,
ambao walikuwa wakiwafadhili kupata mafunzo chuoni hapo, kwa ajili ya
kwenda kujiajiri wenyewe na siyo kutegemea kuajiriwa.
Zoezi
la kukabidhi vifaa hivyo lilifanyika kwenye chuo hicho cha ufundi stadi
VETA, ambapo wahitimu hao walikuwa wamesomea fani za mapishi, Saluni,
Mapambo, Mabomba, Aluminium, umeme, na ufundi pikipiki.
Mratibu
wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam
Katanga, ambao wanajishughulisha na masuala ya kijamii Kanda ya Ziwa,
alisema kuwa wamefadhili mafunzo ya ufundi Stadi kwa vijana 200 kutoka
mkoani Shinyanga ili kuwapatia ujuzi na kuendesha maisha yao.
"Shirika
letu baada ya kufadhili vijana hawa mafunzo ya ufundi na kuhitimu,
tukaona ni vyema kuwaunga kwenye vikundi vya ujasiriamali na kuvisajili,
na kuwapatia vifaa ambavyo wataanza navyo kujiajiri wenyewe kulingana
na fani zao," alisema Katanga.
“Vifaa
ambavyo tumetoa ni vya Mapishi, Saluni, ushonaji zikiwamo cherehani,
ufundi umeme, Aluminium, Mapambo, Mabomba, na pikipiki, ambavyo vijana
hawa vitawasaidia kuanzisha shughuli zao na kujipatia kipato, kuliko
kurudi nyumbani kukaa kusubiri ajira na hatimaye kupoteza ujuzi
wao,”aliongeza.
Naye
Afisa Vijana kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles
Ruchagula, aliwataka vijana hao licha ya kusajili vikundi vyao, wasisite
kwenda kuomba mkopo halmashauri fedha za asilimia 10, ambazo nne kwa
vijana zitakazowasaidia kupanua mitaji yao.
Kwa
upande wake Msajili wa wanafunzi Chuo cha Ufundi stadi VETA mkoani
Shinyanga Rashid Ntahigiye, aliwataka vijana hao wanapoingia kwenye Soko
la kujiajiri wenyewe, wakawe wabunifu kwenye utengenezaji wa bidhaa
zao, ili wafanikiwe kupata wateja wengi na kuinuka kiuchumi.
Nao
baadhi ya wahitimu hao akiwamo Magreth Zabron aliyesomea fani ya
saluni, walishukuru Shirika hilo kuwafadhili mafunzo hayo pamoja na
kuwapatia vifaa vya kuanza kazi, na kuahidi kwenda kujituma kuchapa kazi
kwa ajili ya mustakabali wa maisha yao, na hawato waangusha.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mratibu
wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam
Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya ushonaji kwa ajili ya
kwenda kujiajiri wenyewe.
Mratibu
wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam
Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya Aluminium, ili kwenda
kujiajiri wenyewe.
Mratibu
wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam
Katanga, akikabidhi vifaa kwa wahitimu wa fani ya mapambo na salooni ili
kwenda kujiajiri wenyewe.
Zoezi la kubidhi vifaa likiendelea.
Zoezi la kubidhi vifaa likiendelea , kwa wahitimu wa fani ya mapishi.
Watendaji
wa shirika la VSO, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa
Serikali manispaa ya Shinyanga na chuo cha ufundi stad VETA Mkoani
Shinyanga, wakwati wa hafla ya kukabidhi vifaa kwa wahimitu wa fani
mbalimbali chuoni hapo. waliofadhiliwa masomo yao na VSO.
Picha ya pamoja wahitimu wa VETA, watendaji wa Shirika la VSO, watumishi wa Serikali na VETA.
Mratibu
wa mradi wa kuwezesha vijana kiuchumi kutoka Shirika hilo la VSO Josam
Katanga, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wahitimu
wa mafunzo VETA.
Msajili
wa wanafunzi chuo cha ufundi stadi VETA mkoani Shinyanga Rashidi
Ntahigiye, akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhi vifaa kwa wahitimu
chuoni hapo waliofadhiliwa mafunzo yao na Shirika la VSO.
Afisa
vijana kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga Charles Ruchagula,
akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa wahitimu VETA.
Afisa mtendaji wa Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga Joshua Masengwa, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Afisa
maendeleo Kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga Wema Mashaka,
akizungumza kwenye hafla hiyo ya kukabidhiwa vifaa wahitimu wa VETA.
Wahitimu
wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stadi VETA Mkoani Shinyanga
waliofadhiliwa masomo yao na Shirika la VSO, wakiwa kwenye hafla ya
kukabidhiwa vifaa kwa ajili ya kwenda kujiajiri.
Wahitimu
wa fani mbalimbali kutoka chuo cha ufundi stad VETA Mkoani Shinyanga

Na Marco Maduhu- Shinyanga.
Post A Comment: