Monday, 23 November 2020

KIFAHAMU CHUO CHA MADINI ARUSHA NA KOZI WANAZOTOA

 

Kituo cha Jemolojia Tanzania ( TGC ) ni Kituo cha Serikali, Kipo chini ya Wizara ya Madini,kinatoa mafunzo na huduma mbalimbali katika fani za uongezaji thamani madini.

Kituo kinatangaza nafasi za mafunzo ya muda mfupi katika fani za ukataji na ung'arishaji madini ya vito (Lapidary ) , Sayansi ya madini ya Vito (Gemmology), Usonara (Jewellery design and jewellery manufacturing).

 Kituo kimesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa namba ya usajili REG/SAT/033 kutoa mafunzo katika ngazi za.

 

1. Basic Technician Certificate in Gem and Jewellery Technology (NTA Level 4)

2. Technician Certificate in Gem and Jewellery Technology (NTA Level 5)

3. Ordinary Diploma in Gem and Jewellery Technology (NTA Level 6) 

 

Mafunzo haya yatatolewa katika Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) ambacho kipo Jijini Arusha katika barabara ya Themi-Njiro mkabala na Ofisi ya Afisa Mkazi Madini Arusha.

 Mawasiliano +255272543241 Simu 0737816121 Email: tgc@madini.go.tz  Tovuti: www.tgc.ac.tz

Katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof  Simon Masanjila Akiwa kwenye picha ya Pamoja na Watumishi wa Kituo cha Jemolojia Arusha TGC alipotembelea kituo hicho mapema hivi karibuni.


No comments:

Post a Comment