Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-Up (WOWAP) Issah Shayo akitoa Elimu ya Uraia ya Mpiga Kura kwa Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) jana.

Mtumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) Isack Joramu, akiuliza swali kwa watendaji wa WOWAP (hawapo pichani).
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) wakiangalia vipeperushi vya Shirika hilo vinavyoelekeza kanuni za uchaguzi.

Afisa Utawala wa Shirika hilo, Loveness John akiwakabidhi vipeperushi vyenye ujumbe mahususi wa Elimu kwa Mpiga Kura 2020, kwa wananchi waliofika kupata matibabu Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) 

Afisa Utawala wa Shirika hilo, Loveness John akimkabidhi vipeperushi hivyo Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Senge, Benjamin Mayengera kwa niaba ya walimu wa shule hiyo.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo, akimkabidhi vipeperushi hivyo Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Sabasaba, Grace Benjamini kwa niaba ya walimu wa shule hiyo.
 Afisa Utawala wa Shirika hilo, Loveness John, akitoa  Elimu ya Uraia ya Mpiga Kura kwa  Walimu wa Shule ya Msingi Sabasaba. 

 Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo akitoa Elimu ya Uraia ya Mpiga Kura kwa Watumishi wa Ofisi ya Mkoa wa Singida.


Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-Up (WOWAP) Issah Shayo akitoa mafunzo hayo kwa Watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida.

Watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Watumishi wa Hospitali ya Mkoa wa Singida, wakifuatilia mafunzo hayo.


Mwalimu Angela John wa  Shule ya Msingi Sabasaba, akiuliza swali  kwaWatendaji wa WOWAP wakati wa mafunzo hayo.

 Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo akitoa Elimu ya Uraia  ya Mpiga Kura kwa Walimu wa  Shule ya Msingi Bomani.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo, akimkabidhi vipeperushi hivyo Mwakilishi wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Tigo, Basil Pesambili kwa niaba ya wenzake.
Afisa Tathmini na Ufuatiliaji wa Shirika lisilo la Kiserikali la Women Wake-up (WOWAP) Issah Shayo, akimkabidhi vipeperushi hivyo Msaidizi wa Meneja wa Kampuni ya Simu ya Airtel, Remmy Aloyce kwa niaba ya wenzake. Kulia ni Afisa Utawala wa WOWAP, Loveness John.
Afisa Utawala wa WOWAP, Loveness John,  akitoa Elimu ya Uraia ya Mpiga Kura  kwa Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida (Mandewa) 


Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida


SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Women Wake-Up (WOWAP) limekumbusha jamii kuhakikisha ifikapo Oktoba 28 mwaka huu kila mwenye sifa ya kupiga kura ajitokeze na kadi yake ya kupigia kura katika kituo alichojiandikisha ili kutimiza haki yake ya msingi ya kikatiba

Aidha, shirika hilo limesisitiza umuhimu wa kila mtanzania kuzingatia misingi ya amani na utulivu wakati mchakato huo ukiendelea, ikiwemo kufika mapema kituoni kupiga kura na kuondoka kuendelea na majukumu mengine kwa mujibu wa sheria za uchaguzi, ili kuepusha madhara au viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyoweza kujitokeza

Afisa Utawala wa WOWAP, Loveness John aliyasema hayo kwa nyakati tofauti jana wakati akielimisha na  kukumbusha jamii mkoani hapa juu ya namna bora ya kufanikisha Uchaguzi wa mwaka huu

“Mafanikio ya uchaguzi wa mwaka huu yatatokana na ushiriki wenu, niwasihi sana jitokezeni kwa wingi siku ya octoba 28 ili kwa pamoja tutimize haki ya msingi nay a kikatiba ya kuchagua viongozi bora kwa hatma ya maisha yetu na Taifa letu…’Kura yako ni Sauti yako’,” alisema John

Akizungumza na watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Singida, Makampuni ya Mitandao ya simu (Tigo na Airtel) Hospitali ya Mkoa na Rufaa, walimu wa shule ya Sekondari Senge na shule za msingi Sabasaba na Bomani, Afisa Tawala huyo, alisema kila mdau akitimiza wajibu wake kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa basi watanzania wataweza kupiga kura kwa amani siku hiyo ya uchaguzi

Kwa upande wake, Afisa Tathmini na Ufuatiliaji kutoka WOWAP, Issah Shayo, aliwatoa hofu wapiga kura wote wenye mahitaji maalumu, akisisitiza kuwa tayari maelekezo yametolewa kwa watendaji wote wa uchaguzi kutoa kipaumbele vituoni kwa watu wenye ulemavu, wajawazito, wazee, wagonjwa na akinamama wanaonyonyesha 

Shayo alisema kwa wale wasiojua kusoma na kuandika ruksa kwenda na watu wanaowaamini kwa ajili ya kuwasaidia kupiga kura, lakini pia kumewekwa utaratibu madhubuti na utakaokuwa na tija kwa watu wa makundi maalumu, katika kuhakikisha wote wenye sifa ya kupiga kura wanafanya hivyo, lengo ni kuufanya uchaguzi wa 2020 kuwa wa kuaminika, kwa uwiano na mazingira sawa 

Share To:

Post A Comment: