MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdiely Makange akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuwataka watanzania kumpigia kura za kishindo Rais Dkt John Magufuli kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo hapa nchini
MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdiely Makange akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu kuwataka watanzania kumpigia kura za kishindo Rais Dkt John Magufuli kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo hapa nchini

MWENYEKITI wa zamani wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga (UVCCM) Abdiely Makange amewataka wakazi wa mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuchagua viongozi wa chama cha Mapinduzi(CCM) akiwemo Rais Dkt John Magufuli ili kuhakikisha mkakati wa serikali ya chama tawala ya kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi unafanikiwa


Makange aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisemaserikali ya awamu ya tano ilifanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi katika mkoa huo kwa kuimarisha miundo mbinu mbalimbali ikiwemo Bandari,Barabara,Reli na Umeme.

Alisema takribani shilingi Bilioni 372 zilitolewa na serikali kwa ajili ya kuongeza kina cha maji kwenye Bandari ya Tanga hatua ambayo imewezesha Meli kubwa kutoka ndani na nje ya nchi kutia nanga kwenye Bandari hiyo.

"Tunaona ambavyo sasa wafanyabiashara wa soko kama mgandini na mengineyo ambayo wanauza bidhaa zao kwenda Zanzíbar Meli ya Azam inatia nanga kwenye bandari ya Tanga na kununua biadhaa mbalimbali kutoka Tanga",alisema.

Kwa mujibu wa Kiongozi huyo ni kwamba azma ya serikali yaawamu ya tano kufanya Tanzania kuingia kwenye uchumi wa kati imefanikiwa hivyo ni jukumu la kila mwananchi kuhakikisha kwamba mafanikio hayo yanakuwa endelevu na njia pekee ni kwa kupiga kura na kuwachagua wagombea CCM.

Makange alisema ipo miradi mkubwa mkoani humo ambayo inapaswa kumalizwa chini ya Uongozi wa Mgombes Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli ikiwemo ule wa ujenzi wa Barabara ya Tanga,Pangani,Saadan mpaka Bagamoyo pamoja na ule wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka mkoani Tanga.

"Ndugu zangu njia pekee ya kufanya maendeleo hayo yawe endelevu ni kuchagua wagombea wa CCM kuanzia Rais,Wabunge na Madiwani....tujitokeze kupiga kura kwa maslahi mapana ya hatma ya mkoa wetu...",alisisitiza.

Hata hivyo alisema bado Taifa linahitaji amani na utulivu na chama pekee ambacho viongozi wake wameienzi amani tangu kupata Uhuru mwaka 1961 ni CCM pekee.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: